• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

UJENZI WA JENGO LA MIONZI HOSPITALI YA WILAYA UTETE

Start Date: 2021-10-28
End Date: 2022-06-25


 

Katika mpango wake wa fedha za bakaa za Mapato ya ndani, Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji ilitenga Kiasi cha Shilingi 40,000,000.00 kujenga Jengo la Mionzi katika Hospitali ya Wilaya ya Utete.  Lengo la mradi huu ni kutoa huduma za mionzi katika Hospitali ya Wilaya na kuwaondolea adha Wananchi wanaosafiri umbali mrefu kwenda Wilaya za jirani hasa Kibiti (Hospitali ya Mchukwi) na Mkuranga kwa ajili ya  kufuata huduma hii. Hata hivyo Jengo lililokuwa linatumika hapo awali lilikuwa chakavu sana  hivyo kushindwa kuhimili kutumika kwa ajili ya kutoa huduma hiyo. Ndipo Mkururugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwa kuliona hilo  aliamua kutoa fedha za zilizovuka  mwaka wa fedha 2020/2021  ili ziweze kutumika kujenga Jengo jipya la mionzi.

Ujenzi wa Jengo la mionzi  ulianza tarehe 28.10.2021 na ulitakiwa kukamilika mnamo tarehe 20.03.2022 hata hivyo kikao cha Kamati ya ujenzi cha tarehe 12.04.2022 kilikubaliana kuongeza muda wa kukamilisha mradi huu mpaka tarehe 25.06.2022.

 

Mradi umechelewa kukamilika kutokana na mabadiliko yaliyotokea kwenye ‘structure’ nzima ya Jengo wakati wa utekelezaji wa Mradi. Awali ilikusudiwa kujenga chumba cha mionzi tu ili huduma ianze kutolewa.  Lakini changamoto iliyojitokeza ni ugumu wa uezekaji kwa vyumba vichache ambavyo ni sehemu ndogo tu ya Jengo zima, ambapo ingetulazimu kubomoa tena baada ya kukamilisha eneo liliobaki la Jengo.

 

Hata hivyo ili kutatua changamoto hiyo, kamati ya ujenzi kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji ilipeleka ombi kwenye Kamati ya fedha, Mipango na Utawala ya Halmashauri la kubadilisha matumizi ya  kiasi cha Shilingi 100,000,000.00  zilizokuwa zimetengwa hapo awali kwa ajili ya ununuzi wa mashine ya mionzi zitumike kukamilisha ujenzi wa jengo zima la mionzi badala ya kujenga vyumba vichache tu kama ilivyoelezwa hapo juu. Kamati ya Fedha, Mipango na Utawala iliridhia ombi hilo, hivyo kufanya jumla ya gharama za mradi wa Jengo la mionzi mpaka utakapokamilika kuwa Shilingi 140,000,000.00

 Mradi huu unatekelezwa kwa mfumo wa “force account”. Ambapo Fundi aliyeshinda zabuni ni Jeshi la Magereza Utete. Mpaka sasa kiasi cha Shilingi 32,276,000,00 zimetumika ikiwa  malipo ya fundi ni Shilingi 3,500,000.00 na  ununuzi wa vifaa vya ujenzi kiasi cha Shilingi 29,276,000.00.

 

Kamati ya ujenzi inatoa shukurani za dhati kwa Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwa kufanya ufuatiliaji wa karibu wa mradi huu na kuhakikisha wataam na wakuu wa Idara wanaohusika na mradi huu wanafanya ufuatilaji wa karibu na  kutatua changamoto zinazojitokeza ili mradi uweze kukamilika kwa wakati.

 Pia tunawashukuru wataalam kutoka OR – TAMISEMI pamoja na majukumu mengi mliyokuwa nayo lakini mmefika katika Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji hasa Hospitali ya Wilaya - Utete na kujionea mazingira yetu ya utendaji kazi.

  

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • SIRI YA RUFIJI KUMSHUKURU RAIS SAMIA NA MBUNGE MCHENGERWA

    May 09, 2025
  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa