• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

Mifugo na Uvuvi

I:     MAELEZO MAFUPI KUHUSU IDARA

Idara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ni moja ya Idara 13 zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Rufiji. Idara ina vitengo vikubwa 2 (Mifugo na Uvuvi) ikiwa na jumla ya watumishi 23 ambapo 20 ni wanaume na 3 ni wanawake. Kitengo cha Mifugo kina watumishi 16 (ambapo wanaume wapo 13 na wanawake 3) na kitengo cha Uvuvi wapo watumishi 7 na wote ni wanaume na kitengo cha Uvuvi kina watumishi 7 (4 wapo Makao Makuu na 3 katika vizuia vya Tarafa 3).

Kufuatana na Ikama, wataalamu wa kitengo cha Mifugo wanaohitajika ni 72 (16 wa Makao Makuu, 13 katika ngazi ya Kata na 43 katika ngazi ya Kijiji/Kitongoji). Hivyo, upungufu ni wataalamu 56 (12 Makao Makuu, 4 ngazi ya kata na 35 ngazi ya vijiji na 5 katika vitongoji vya mji mdogo).

Kufuatana na Ikama, watumishi wa Kitengo cha Uvuvi wanaohitajika ni 23 (10 makao makuu, 9 katika Tarafa, madareva wa Boti 2, na mafundi wa Boti 2). Hivyo, upungufu ni watumishi 16 (6 Makao Makuu, 6 katika ngazi ya Tarafa, Madareva wa Boti 2, na Mafundi wa Boti 2).

Shughuli zinazofanywa na Idara kwa ufupi ni kama zifuatazo:

  • Ukusanyaji wa takwimu mbalimbali za Mifugo na Uvuvi na kuzihifadhi katika mfumo maalum wa takwimu kwa matumizi ya maendeleo ya Idara,
  • Ushauri wa ufugaji bora wa Mifugo na Samaki hasa katika mabwawa,
  • Utoaji wa Elimu ya ufugaji wa kisasa kwa wafugaji wa Mifugo na Samaki,
  • Matibabu ya magonjwa ya Mifugo na Samaki,
  • Usimamiaji wa shughuli za minada ya Mifugo,
  • Ukaguzi wa Mifugo inayochinjwa na inayokufa kabla ya kuchinjwa,
  • Ukaguzi wa ubora na usafi masoko ya Samaki,
  • Ukaguzi wa maduka ya madawa ya Mifugo na viwanda vya kutengeneza vyakula/mabaki yatokanayo na mifugo,
  • Usimamizi wa Sheria na Kanuni za Mifugo na Uvuvi,
  • Ukusanyaji wa mapato yatokanayo na vyanzo vya sekta ya Mifugo na Uvuvi na kubuni vyanzo vipya vya mapato.
  • Kuandaa mipango ya Maendeleo ya Halmashauri ya muda mfupi na ya muda mrefu kwa sekta za Mifugo na Uvuvi pamoja na kuhusisha sekta mtambuka.
  • Kushughulikia migogoro baina ya wakulima na wafugaji kwa kushirikiana na Sekta za Kilimo, Ardhi na Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Idara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, ina fursa za uwekezaji mbalimbali lakini kutokana na jamii kukosa uelewa wa uwepo wa fursa katika sekta za Mifugo na Uvuvi, hakuna wawekezaji ambayo wamejitokeza katika kuzitumia fursa hizo kwa ajili ya kuendeleza Sekta hizo.

Zilizoainishwa hapa chini ni baadhi ya fursa za uwekezaji katika sekta za Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri ya wilaya ya Rufiji.

II:       FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MIFUGO

Halmashauri ya wilaya ya Rufiji inakisiwa kuwa na takriban Ng’ombe 100,000 hadi kufikia Januari 2017. Mbali ya kuwa na Ng’ombe kiasi hicho, Halmashauri ina idadi ndogo sana ya Miundo Mbinu ya Mifugo kama vile Majosho, Vituo vya Afya vya Mifugo, Machinjio, Mabanda ya ngozi, Malambo, Njia za kupita Ng’ombe, Vibanio. Eneo hili kwetu tunaliona ni eneo muhimu sana la kipaumbele katika kuboresha afya ya Mifugo, kipato cha Halmashauri na uwekezaji kwa watu binafsi au kampuni. Hivyo, wawekezaji mbalimbali mnakaribishwa sana kuwekeza katika Sekta hii aidha kwa kushirikiana na wafugaji au Halmashauri ili kuchangia katika uchumi wa mwananchi wa Rufiji, wilaya na Taifa kwa ujumla. Maeneo mengine ambayo ni fursa katika sekta ya mifugo ni:

  • Kiwanda cha Nyama: 

Wilaya haina machinjio hata moja, kilichopo ni makaro ya kuchinjia Ng’ombe na Mbuzi ambayo yapo takriban 6. Hivyo, kuna haja ya kujenga machinjio katika wilaya kwa lengo la kupata nyama safi na salama zaidi ambayo thamani yake itakuwa kubwa kuliko ilivyo sasa.

  • Utengenezaji wa Ngozi:  

Kwa ajili ya kuongeza thamani ya ngozi kwa kutayarisha ngozi kwa ajili ya viwanda vingine au watumiaji wengine, kuna haja ya kuwa na mabanda ya kisasa au njia bora za uandaaji wa ngozi katika maeneo yanayochinja mifugo. Hii ni fursa kwa kuwa, itasaidia kuongeza kipato kwa Serikali kuu, Halmashauri na kuongeza ajira kwa wakazi wa Rufiji.

  • Vituo vya Mifugo na Maduka ya Dawa za Mifugo: 

Fursa nyingine ni uanzishaji wa Maduka ya dawa za mifugo ya kisasa kwani wataalamu wa mifugo wapo, utoaji wa huduma za ushauri kwa wafugaji na uanzishwaji wa vituo vya afya ya mifugo kwa ajili ya kukagua afya yao na kuwezesha kugundua magonjwa ya mlipuko mapema. 

  • Uanzishwaji wa viwanda vya kutengeneza vyakula vya Mifugo:

Wilaya haina hata kiwanda kimoja cha kutengeneza chakula cha mifugo iwe Ng’ombe, Mbuzi, Kuku, Nguruwe, Mbwa nk. Vyakula vingi vinanunuliwa toka Dar Es Salaam ambapo ni km 240 toka makao makuu ya wilaya. Kumekuwa na ongezeko kubwa la mifugo kuingia ndani ya wilaya na hivyo tunaatarajia kuwepo na mahitaji makubwa katika miaka isiyozidi 5. Hili linasababishwa na kujengwa kwa viwanda katika mikoa ya jirani ya Lindi na Mtwara pamoja na wilaya ya Mkuranga na hivyo kutokana na matarajio ya ongezeko la watu watakaoajiriwa kuwa na kuongeza mahitaji ya Nyama, Maziwa, Mayai nk.

  • Viwanda vya kusindika Maziwa:

Halmashauri ya wilaya ya Rufiji kwa sasa hivi inazalisha wastani wa lita 2,000 litres of Maziwa kwa siku lakini ni lita 300 tu ndio ambazo zinasindikwa na kupelekwa kuuzwa Mkoa wa Dar Es Salaam. Hili linafanywa na kiwanda kimoja kidogo cha Manyonyo Dairies. Hivyo, fursa ipo katika uanzishwaji wa viwanda vya kusindika Maziwa na uanzishwaji wa mnyororo wa thamani wa Maziwa. Vilevile, kuna haja ya uanzishwaji wa vituo vya kukusanyia maziwa kutoka maeneo yanayozalisha ili kuweza kupata maziwa safi na bora zaidi. Kwa kufanya hivi, itawezesha vijana kupata ajira, wilaya kupata mapato, mfugaji kupata kipato na uboreshaji wa ufugaji wa Ng’ombe na Mbuzi wa maziwa.

  • Minada ya Upili: 

Kuna minada 3 ya Mifugo katika Halmashauri lakini hakuna mnada hata mmoja ni wa kisasa. Minada yote imejengwa kwa miti na haina ramani ya kueleweka. Mbali ya kuuzwa Ng’ombe takriban 2,000 na Mbuzi 1,500 kila wiki, udhibiti bado sio mzuri na hivyo huwa tunapoteza mapato. Juhudi zinafanywa ili kupata wawekezaji ambao watasaidia au watawezesha ujenzi wa minada ya kisasa kwa ubia na Halmashauri ili kudhibiti ukusanyaji wa mapato. Hii ni fursa kwa wawekezaji mbalimbali na vilevile kwa wajasiriamali wa vyakula, nguo, spea za baiskeli na pikipiki, vinywaji mbalimbali, maduka ya kutembeza vifa mbalimbali.

III:  FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA UVUVI 

Katika Wilaya ya Rufiji, uvuvi unafanyika kwenye mto Rufiji na mabwawa ya asili 13 yanayojazwa na maji ya mafuriko ya mto Rufiji.

Kuna wavuvi wadogo 1950 waliojiajiri kwenye shughuli ya uvuvi na wanatumia mitumbwi yenye ukubwa wa kati ya mita 3-11 na inaendeshwa kwa kasia.

Samaki wanaozalishwa ni pamoja na kumba, pele, ngocho, kasa, kambale, kitoga. Pia kuna mabwawa ya kuchimba ya watu binafsi 13 ambao wanafuga samaki aina ya perege. Baadhi ya fursa za uwekezaji ni kama ilivyoainishwa hapa chini.

Ufugaji wa samaki;

Kuna maeneo mazuri ya kuchimba mabwawa na hali ya hewa nzuri kwa ajili ya ufugaji wa samaki aina ya tilapia na kambale, fursa zilizopo katika ufugaji wa samaki ni;-

  • Uanzishwaji wa vituo cha kuzalisha mbegu bora za samaki na vyakula vya samaki, kituo cha kuzalisha mbegu za samaki Rufiji kwa sasa hakuna. Hivyo kuna changamoto katika kuendeleza ufugaji wa samaki katika mabwawa ya kuchimba kwa sababu mbegu zinapatikana maeneo ya mbali (kama Dar es Salaam, Bagamoyo na Morogoro) takriban kilomita zaidi ya 240.
  • Hakuna kiwanda cha uchakataji, usindikaji na uongezaji wa thamani wa mazao ya uvuvi kwa ajili ya masoko ya ndani na nje. Mazao yanayozalishwa huwa yanaharibika mapema baada ya kuvuliwa hivyo kumfikia mlaji wa mwisho yakiwa kwenye hali mbaya au yanaharibika kabisa kiasi cha aidha kutofaa kutumika au kununuliwa kwa bei ndogo sana.
  • Ujenzi wa soko la kisasa la mazao ya samaki. Masoko yaliyopo katika maeneo ya Ikwiriri, Utete, Mohoro hayana miundombinu mizuri ya kuuzia mazao ya uvuvi, hivyo mazao kupoteza soko la kuuzika kwa sababu yanakuwa kwenye hali ambayo sio ya usafi.

Vitendea kazi vya uvuvi na tekinolojia;

  • Utengenezaji, ununuzi na usambazaji wa zana za uvuvi kwa vikundi vya wavuvi (kama vile nyavu bora za kuvulia, vifaa vingine vya uvuvi, vifaa vya usalama & tahadhari katika mitumbwi/boti). 
  • Matumizi ya teknolojia ya kisasa katika utengenezaji wa vyombo vya kisasa vya uvuvi kwa kutumia malighafi iliyopo Rufiji tofauti na mbao ambavyo vitakuwa salama zaidi ya vyombo wanavyotumia wavuvi.
  • Wavuvi wanapoenda kuvua huwa hawana vifaa vya kuhifadhia samaki (mabox maalum ya barafu) ili wasiharibike lakini vilevile hata wanapofika ufukweni hakuna eneo lolote la kuhifadhi samaki hao kama majokofu. Kutokuwepo kwa vifaa hivyo kunapunguza sana thamani ya samaki katika masoko na viwanda vya kuchakata samaki wanakopelekwa.

IV:       CHANGAMOTO ZA IDARA

A: SEKTA YA MIFUGO

  • Uhaba wa Miundo Mbinu ya Mifugo kama vile Malambo, Minada, Majosho na vibanio katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ufugaji;
  • Uhaba wa maeneo ya malisho kutokana na kwamba zaidi ya asilimia 50 ya vijiji havijafanyiwa Mpango wa matumizi bora ya ardhi;
  • Uhaba wa masoko ya uhakika kwa ajili ya maziwa, mayai na nyama;
  • Mwitikio mdogo wa wafugaji katika matumizi ya kanuni bora za ufugaji wenye tija na maendeleo kwa jamii;
  • Uhaba wa vitendea kazi kama gari, Pikipiki kwa Maafisa ugani ambavyo vinarahisisha utendaji kazi na kuleta ufanisi;
  • Idadi ndogo ya wataalamu wa mifugo haukidhi kuhudumia jamii yote ya wafugaji kama Sera ya Mifugo inavyoagiza.

B: SEKTA YA UVUVI

  • Ongezeko la Uvuvi haramu wa kutumia nyavu zenye macho madogo hivyo kusababisha samaki wachanga wanavuliwa kwa wingi, matumizi ya baruti, mabomu na sumu (hasa dawa za mimea na mifugo);
  • Uhaba wa vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya kufanya sensa katika mto Rufiji na mabwawa ili kupata takwimu sahihi za aina mbalimbali za samaki na umri/ukubwa wao;
  • Uhaba wa vitendea kazi kama gari, pikipiki kwa ajili ya kuwezesha kufanya doria za mara kwa mara katika mito na mabwawa;
  • Sekta haijawekewa kipaumbele cha maendeleo kwani haitengewi bajeti ya maendeleo na Serikali na vilevile haitengewi bajeti ya matumizi ya uendeshaji wa Sekta na dharura. Kwa kutokufanya hivyo, kunasababisha wataalamu wa uvuvi kutotumika ipasavyo katika kuendeleza sekta hii kwani fedha za mgao wa kutoka Halmashauri ni ndogo sana. Ukiainisha vizuri, sekta hii ina uwezo wa kuongeza kipato cha mwezi na mwaka kwa mwananchi wa Rufiji, kuongeza kiwango cha protini itokanayo na wanyama na ambayo haina madhara ya madawa, kuhifadhi ardhi ambayo si rafiki kutumika kwa ajili ya Kilimo/Mifugo/Makazi nk, na ina uwezo wa kutoa ajira mbalimbali kwa vijana, wanawake, wazee hata kama hawajahitimu madarasa ya shule za msingi/sekondari.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA AMWAGA BIL. 50 BARABARA YA IKWIRIRI -MKONGO

    June 23, 2025
  • DC KOMBA AAGIZA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI ITOLEWE KWA KATA ZOTE RUFIJI.

    June 26, 2025
  • WATUMISHI WA UMMA RUFIJI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI, WASISITIZWA KUFANYAKAZI KWA BIDII, WAONYWA KUTOA HUDUMA KWA UPENDELEO MAOFISNI

    June 25, 2025
  • BEREGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA MKONGO, KIPUGIRA, NGORONGO

    June 11, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa