• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

TAARIFA YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA NGARAMBE

Start Date: 2022-04-02
End Date: 2022-07-02


 

Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ilipokea Fedha kiasi cha Shilingi. 250,000,000.00 kutoka Serikali Kuu (Fedha za Tozo ya miamala ya Simu), kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Ngarambe. Fedha hizi zilielekezwa kujenga Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD), Jengo la maabara pamoja na  kichomea taka.

Ujenzi wa Kituo cha Afya Ngarambe ulianza tarehe 02/04/2022 kwa majengo mawili yaani Jengo la Wagonjwa wanje (OPD) na Maabara, na unatarajiwa kukamilika mnamo tarehe 02/07/2022. Mafundi waliopewa kazi ni Faridu Mbulu na Modestus Kayombo. Mpaka sasa fedha iliyotumika ni Shilingi 67,320,000.00 kwa ununuzi wa vifaa na malipo ya mafundi. Nguvu za wananchi katika utekelezaji wa mradi huu inakadiriwa kuwa Kiasi cha Shilingi 4,650,000.00 kwani walijitolea ardhi yenye ukubwa wa ekari kumi (10) na kusafisha eneo la ujenzi. Vilevile wananchi wanajitolea kusimamia utekelezaji wa mradi huu kupitia kamati mbalimbali za ujenzi zilizoundwa ambapo wao ni wajumbe wa kamati hizo. Fedha iliyobaki mpaka sasai ni kiasi cha Shilingi. 182,680,000.00.

 Mpaka sasa Jengo la maabara  lipo hatua linta na  Jengo la OPD lipo hatua ya kuinua kuta.

Ujenzi wa Kituo cha Afya Ngarambe utasaidia sana Wananchi wanaosafiri umbali wa kilometa zaidi ya sitini (60km) kwenda kutibiwa katika hospitali ya Wilaya iliyopo Utete. Pia itasaidia sana kupata   huduma za dharula kwa Wajawazito.  Hivyo tunategemea kupunguza sana vifo kwa kina Mama wajawazito na Watoto chini ya miaka mitano mara tu Kituo kitakapokamilika na kuanza kufanya kazi.

 

Changamoto kubwa iliyopo katika utekelezaji wa mradi huu ni ubovu wa miundombinu hasa barabara, ambayo inaleta ugumu katika usafirishaji wa vifaa vya ujenzi. Hali hii inapelekea kupanda kwa gharama ya usafirishaji wa vifaa vya ujenzi mpaka eneo la mradi na kusabisha mabadiliko ya gharama zinazokuwa zimekadiria hapo awali. Hata hivyo wananchi wamekuwa wanajitolea hata kubeba vifaa vya ujenzi kwa kutumia baiskeli pale gari inaposhindwa kufikisha vifaa hivyo eneo la mradi kutokana na ubovu wa barabara.

Changamoto nyingine kubwa ni ukosefu wa maji karibu na eneo la mradi ambapo maji yanapatikana umbali wa zaidi ya kilomita 3 kutoka eneo la mradi. Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji imetoa guta (pikipiki ya miguu 3) ili iweze kusaidia kuchota maji na kuhakikisha yanapatikana muda wote katika eneo la Mradi.

 Wananchi wa Kata ya Ngarambe tunapenda Kumshukuru sana Mkururgenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwa ufuatilaji wa mara kwa mara na kuhakikisha wataalamu wa Halmashauri wanakuwepo eneo la mradi bila kujali umbali uliopo Zaidi ya kilomita 60 kutoka makao makuu ya Wilaya. Pia tunapenda kumshukuru Mh. Mbunge wetu wa Jimbo la Rufiji kwani amekuwa akitutembelea kila anapopata nafasi na kutuhimiza kusimamia vizuri mradi huu ili uweze kuleta tija kwetu. Tunapenda kuwashukuru wageni wetu kwa kuweza kufika katika Kata ya Ngarambe bila kujali umbali wala changamoto iliyopo ya ubovu wa barabara.

 Mwisho kabisa tunapenda kumshukuru Mh.Rais  Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea mradi huu mkubwa katika katika Kata yetu. Ama kwa hakika kama jina lake ametuletea, suluhisho la ukosefu wa huduma bora za Afya kwa Zaidi ya miaka 60 tangu kupata Uhuru.

Baada ya kusema hayo tunawaomba wageni wetu mpite na kukagua maendeleo ya ujenzi.

Matangazo

  • TANGAZO LA MIKOPO YA VIKUNDI July 21, 2022
  • TANGAZO LA USHIRIKI WA MAZOEZI YA VIUNGO September 08, 2022
  • TANGAZO LA JKT 2022 August 30, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA YA HALMASHAURI August 24, 2022
  • Ona zote

Habari Mpya

  • DC GOWELE AIPONGEZA HALMASHAURI KWA KUWATETEA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI

    January 27, 2023
  • MWENYEKITI WAZAZI CCM TAIFA ASIFU UTENDAJI WA SERIKALI RUFIJI, AWATAKA KUSIMAMIA MIRADI

    January 28, 2023
  • KAMATI YA FEDHA, MIPANGO NA UTAWALA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

    January 27, 2023
  • BARAZA LA WAFANYAKAZI LARIDHIA MAPENDEKEZO YA MPANGO WA BAJETI 2023/2024

    January 27, 2023
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa