• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

Wazazi wapatieni mahitaji ya shule watoto - Kiongozi Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018

Posted on: July 13th, 2018

"Wazazi na walezi wapatieni mahitaji ya shule watoto" -  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndugu Charles Francis Kabeho. Kiongozi huyo ameyasema hayo wakati akitoa ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Wilayani Rufiji katika viwanja vya chuo cha Maendeleo ya wananchi Ikwiriri. Amesema kuwa Serikali ya awamu ya 5 chini ya Mh. Dr. John Pombe  Magufuli imefuta ada na michango mingine kwa elimu ya awali ya kuanzia chekechea mpaka kidato cha 4. Lakini jukumu la kuwapatia watoto mahitaji ya shule kama sare, daftari, kalamu na penseli bado lipo mikononi mwa wazazi na walezi, hivyo kila mzazi au mlezi ahakikishe anampatia mtoto wake mahitaji muhimu ya shule. Pia wazazi na walezi wameshauriwa kushirikiana kwa ukaribu na walimu kuhakikisha watoto wao wanapata elimu iliyo bora.  Wazazi na walezi wana jukumu la kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muugano wa Tanzania kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora, hivyo kila mmoja hana budi kukagua daftari za mwanae ili kujua maendeleo ya kijana wake kimasomo. Pia ni jukumu la kila mmoja kuchangia upatikanaji wa miundo mbinu ya kufundishia na kujifunzia mfano kuchangia ujenzi au ukarabati wa madarasa, vyoo, nyumba za walimu na viwanja vya michezo.

Ili mtoto aweze kuzingatia masomo na mzazi au mlezi kuwa na uwezo wa kutafuta mahitaji ni lazima wote wawe na afya njema. Hivyo jamii imeshauriwa kuepukana na matumizi ya madawa ya kulevya kama bangi, mirungi, kokeini na mengine yanayofanana na hayo kwani hudhoofisha afya na kusababisha utendaji kazi wa viungo vya mwili kuwa duni. 

VVU/Ukimwi ni ugonjwa unaoendelea kuathiri afya za watanzania walio wengi. Ugonjwa huo huambukizwa kwa nia mbalimbali kutoka kwa mwathirika kwenda kwa mtu mwingine kupitia njia mbalimbali ikiwemo ya kufanya tendo la ndoa na mtu aliyeathirka bila kinga na kuchangia vifaa vyenye ncha kali kama vile wembe na sindano. Serikali bado inaendelea kupambana na ugonjwa huo kwa kuanzisha vituo vya kutolea huduma za VVU/UKIMWI ikiwa ni pamoja na kutoa dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi bila gharama kwa wote wlioathrikia na VVU/UKIMWI. Jamii imeshauriwa kupima na kujua hali ya maambukizi ili kama mwananchi akijikuta tayari ameshaambukizwa aanze kutumia dawa mapema na kama bado basi aendelee kujilinda ili asipatwe na maambukizi hayo.

Malaria ni ugonjwa unaoshambulia wananchi wengi na kusababisha vifo hasa kwa watoto walio chini ya miaka 5 na mama wajawazito. Serikali bado inaendelea na jitihada za kukomesha kabisa ugonjwa wa malaria kwa kuhakikisha kila kituo cha kutolea huduma za afya kinakuwa na vifaa vya kupima  na dawa za kutibu malari. "Siyo kila homa ni malaria" - Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Wilayani Rufiji. Hivyo ameiasa jamii kujenga mazoea ya kupima badala ya kuanza kutumia dawa kabla ya kupima kwani kuna magonjwa mengi ambayo dalili zake zinafanana na malaria.

Rushwa ni adui wa haki, kataa Rushwa - Jenga Uchumi wa Tanzania. Akiongea na wananchi wa Wilaya ya Rufiji Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 amewasisitizia wananchi na watanzania kwa ujumla kukataa rushwa kwani palipo na rushwa haki hukosekana hivyo kupelekea wanyonge kuonewa. Kila mwananchi ameaswa kuwa kiongozi wa kuzuia na kupambana na rushwa katika eneo lake la kazi kwa kutoa taarifa kwa kupiga simu namba 113 ambayo ni bure mitandao yote pale anapoona vitendo vya kupokea au kutoa rushwa vikifanyika.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa