• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

WANACHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA MWEKEZAJI

Posted on: December 30th, 2022






Serikali Mkoani Pwani, imewaasa wananchi wa kata ya Chemchem ,Utete wilayani Rufiji Mkoani Pwani kutoa ushirikiano kwa mwekezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji Sukari Lake Agro sugar estates, unaotarajia kutoa ajira zaidi ya 3,500 na kugharimu dollar za kimarekani milioni 321 ifikapo 2025.



Akitembelea na kukagua eneo la mradi huo leo Desemba 30,2022 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe  Abubakari Kunenge alieleza, kwa upande wa Serikali imembariki mwekezaji huyo kuendelea na mchakato ya uwekezaji kwa manufaa chanya ya kata , wilaya, mkoa na Taifa kijumla.



Alieleza, kiwanda hicho kinakwenda kutatua uhaba wa sukari na kuondokana na uingizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.



Kunenge alieleza, kwasasa mahitaji ya sukari  Nchini (brown sugar) ni tani 440,000 na sukari nyeupe ya Viwandani tani 220,000 , hivyo uwekezaji huo ni mkombozi kwa wanaRufiji.



"WanaRufiji tunafungua mkoa na wilaya hii wapo wenzenu wanalilia wawekezaji kama hawa ni wajibu wetu kuhakikisha tunatoa ushirikiano, Panapokuwa na misuguano hakuna maendeleo, elimu izidi kutolewa jamii ielewe umuhimu wa mradi huu badala ya kuweka vikwazo"



"Huwezi kupata tija kwa kuvutana, mivutano haina manufaa, kwani mradi unahitaji wananchi na wananchi wanahitaji mradi, unapochelewa mradi mnaongeza gharama za mradi kwa mwekezaji na kumpa hasara"alifafanua Kunenge.



Hata hivyo Kunenge alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa matokeo makubwa ya kazi yake inayoonekana kufanyika katika mkoa huo ikiwemo katika uwekezaji, miradi mikubwa ya kimkakati, maji,umeme, miundombinu,elimu na afya



Aidha Kunenge alieleza ni wajibu wa wazazi na walezi Rufiji Mkoani Pwani kuandaa vijana wao ili waje kunufaika na mradi huu.



"Nimetembelea viwanda 28 kila nilipopita wawekezaji wanatoa changamoto ya vijana wazawa kushindwa kuendelea na kazi ,suala ambalo linasikitisha "alibainisha Kunenge.



Naye Meneja mradi Lake Agro,  Abubakar Nassoro alieleza ,wameanza Septemba mwaka 2021, ambapo wapo kwenye hatua ya maandalizi ya vitalu miche ya miwa, wamechimba bwawa la maji linalobeba ujazo wa Lita milioni 4.8,umeme na kuboresha miundombinu mbalimbali.



Alieleza, kiwanda cha sukari kinatarajia kuanza mwaka 2025 kwa kuzalisha tani 300,000 za sukari na pia watatumia kilimo cha mkataba kwa wakulima wa nje.



Nassoro alieleza ,eneo la uwekezaji ni hekta 15,000 ambalo awamu ya kwanza wamefanya tathmini na kulipa fidia kwa Wananchi 42 kiasi cha sh.milioni 172  huku awamu ya pili wanatarajia kuwalipa fidia wananchi 130 na Sasa wapo katika hatua ya kusubiri muongozo wa Serikali.






Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa