• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

Posted on: August 18th, 2017

Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji wakisikiliza kwa makini Taarifa za Mkutano wa mwaka 2016/2017 wa Baraza la Madiwani.

Katika Mkutano huo Waheshimiwa madiwani walihoji mambo kadhaa ili kupata ufafanuzi wa kiutendaji au kitaalam; miongoni mwa mambo hayo yaliyoulizwa na madiwani ni pamoja na:-

Swala la mali chakavu za Halmashauri, ni kwa nini zisiuzwe ili zipatikane pesa kiasi zitumike katika shughuli nyingine za kimaendeleo ndani ya Halmashauri. Akijibu hoja hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji ndg: Rashidi S. Salum alisema kuwa mali chakavu zote za Halmashauri zitapigwa mnada wa hadhara kuanzia tarehe 31 Agosti 2017 hadi 02 Septemba 2017. Tayari tangazo la mnada huo limeshatangazwa kwenye vyombo vya habari yakiwemo magazeti, tovuti ya Halmashauri na ubao wa matangazo wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji. Kwa mwananchi yeyote anayehitaji kupata taarifa zaidi kuhusu mnada huo atembelee ubao wa matangazo au tovuti ya Halmashauri. 

Vitambulisho vya wazee kwa ajili ya kupata huduma ya Afya bado inaonekana ni changamoto baada ya kugundulika kuwa vitambulisho hivyo vimetolewa kwa baadhi ya wazee (560 kati ya 3000) katika kata 3 tu wakati Halmashauri ina jumla ya kata 8. Madiwani walihitaji kujua ni kwa nini kazi hiyo ya kuwatengenezea vitambulisho vya Bima ya  Afya wazee imeonekana kuchukua muda mrefu. Katika kujibu hoja hiyo kaimu mganga mkuu Wilaya ndg: Rasmo Msabaha alisema kuwa idara ya Afya inaendelea kuwasajili wazee ili wpate vitambulisho. Hata hivyo alifafanua kuwa hakuna mzee aliyewahi kutembelea kituo chochote cha kutolea huduma za kiafya akakosa huduma kwa sababu ya kutokuwa na kitambulisho. Alisema kuwa tatizo lililosababisha baadhi ya wazee kuchelewa kupata vitambulisho ni kwa sababu ya baadhi ya vituo vya kutolea huduma kuishiwa kadi maalum kwa ajili ya kutengeneza vitambulisho hivyo; lakini alisisitiza kuwa ufuatiliaji wa kina unaendelea kuhakikisha kwamba karatasi hizo zinapatikana na wazee wanatengenezewa vitambulisho vya Bima ya Afya mapema kabla ya mwezi Desemba 2017. 

Uchaguzi wa Makamu mwenyekiti wa Halmashauri na Kamati za kudumu za Halmashauri. Nafasi ya Makamu mwenyekiti wa Halmashauri iligombewa na mgombea mmoja tu mhe: Hawa Mtopa ambaye ndiye pia alikuwa anamaliza muda wake (mwaka mmoja madarakani) akiwa kama Makamu mwenyekiti.  Hivyo ilimlazimu kujiuzulu kwanza nafasi hiyo na baadae alipigiwa kura za siri za ndiyo au hapana. Kura zilizopigwa zilikuwa kura 16; kati ya hizo ndiyo zilikuwa 10 na hapana 6 hivyo mhe: Hawa Mtopa alifanikiwa kutetea nafasi yake ya Makamu mwenyekiti wa Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Wajumbe wa kamati za kudumu za Halmashauri waliopatikana ni kama ifuatavyo:-

Huduma za jamii

        R. Mtumbange (Mwenyekiti), H. Momboko, L. Mpembenue, S. Mikengesi, A. Ndungutu, N. Chamwenyewe, A. Mduma, K. Kisoma, S. Malenda

Maadili

        S. Mikengesi, K. Kisoma (Mwenyekiti), L. Mpembenue, T. Mapengo, R. Mege

Uchumi, Ujenzi na Mazingira

         J. Ligomba (Mwenyekiti), S. Mbwilani, T. Mapengo, J. Mlanzi, R. Mege, S. Malenda, S. Mtindugo, H. Mtauka 

Ukimwi

          H. Mtopa, H. Mtauka, J. Mlanzi

Fedha

          H. Mtimbuko, A. Ndungutu, Mwenyekiti wa Halmashauri na wenyeviti wa kamati zote za kudumu.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa