• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

WAJUMBE WA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA RUFIJI WAAPA RASMI, WASISITIZWA KUTENDA HAKI

Posted on: March 27th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge, amewaapisha Wajumbe  wa nne wa baraza la ardhi na Nyumba la Wilaya ya Rufiji, litakalokwenda kufanya maamuzi ya migogoro mbalimbali ya ardhi Wilayani humo ili kupunguza migogoro.

Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wajumbe hao, imefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Ikwiriri, jana machi 27, 2024 ambapo Wajumbe walioapishwa ni pamoja na Aminu Lipunda, Zainabu Ngalemera, Salum Kipoloya na Salum Kilemba.

Kunenga, amesema baraza hilo lipo kwa mujibu wa sheria ya utatuzi wa migogoro ya ardhi, huku akiwasisitiza Wajumbe hao kutenda haki kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo na kuwataka kutofanya maamuzi kwa utashi wa Mtu, hali itakayopelekea kupindisha haki.

“licha ya hali ya ubinadamu wenu, mjitahidi kadiri Mungu alivyowajaalia mtende haki, mmeteuliwa kwa mujibu wa sheria, fanyeni kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo tuliyowapa. Msifanye kwa mujibu wa utashi wa Mtu. Rufiji migogoro ya ardhi ni mingi, fanyeni kwa mujibu wa sheria, Mtangulizeni Mwenyezingu mbele” amesisitiza Kunenge.

Amesema uwepo wa baraza hilo litakwenda kupunguza migogoro ya ardhi iliyokithiri Rufiji  huku akiwasisitiza kutenda haki pale wanapofanya maamuzi ya migogoro hiyo.

Vilevile Kunenge, amekemea tabia ya baadhi ya mabaraza ya Kata kufanya maamuzi badala ya kufanya usuluishi ili watu wafikie makubaliano.

“… kazi ya mabaraza ya Kata ni kufanya usuluishi ili kusaidia Watu kufikia makubaliano, na sio kufanya maamuzi” aliongeza Kunenge.


Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amewataka Wajumbe hao kuishi kwenye kiapo walichokiapa ili waende kufuta machozi ya Wanarufiji kwa kutatua kero mbalimbali za migogoro ya ardhi.

“kilio chetu sisi kilikuwa ni kupata baraza hili, naomba mkaishi kwenye kiapo mlichokiapa leo, na sisi tunaamini kupitia ninyi mtaenda kufuta machozi ya Wanarufiji kwenye changamoto walizokuwa nazo” alisema Dc Gowele.

Baraza la ardhi la Wilaya ya Rufiji linakamilisha idadi ya  mabaraza 7 yaliyoundwa Mkoani Pwani ambapo Kwa Wilaya ya Rufiji linabeba historia ya kuwa Baraza la kwanza kuanzishwa na kuwasaidia Wananchi waliokuwa wakikosa haki zao kwasababu ya kushindwa kusafiri kuelekea Wilayani Mkuranga ambapo ndipo walipokuwa wakipata huduma hapo awali.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa