• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

WAFUGAJI WATII AMRI YA MH. SAWALA

Posted on: August 28th, 2020

Ni siku ya ijumaa tar 28/08/2020 katika Ukumbi wa Serengeti mahali amabapo umefanyika Mkutano Mkubwa uliokusanya wafugaji takribani 120 kutoka Rufiji na Washirika wenzao kutoka kibiti, miongoni mwao kukiwa na mfugaji wa kike mmoja tu, huku jemedari wao akiwa ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Asilia Rufiji Ndg. Deus Naki. Akisoma taarifa fupi ya chama hicho katibu wa chama ameeleza kuwa mpaka sasa chama kinawafugaji 262 na changamoto zinazowakabili wafugaji hao ni pamoja na kukosekana kwa njia mahususi za malisho, upungufu wa majosho, ongezeko la idadi ya Mifugo na Watu hasa kuanzia mwaka 2005 – 2009 ambapo kulikuwa na ng’ombe 72530, Mbuzi 13130 pamoja na kondoo. katibu huyo aliendelea kusema kuwa ongezeko la migogoro lilikithiri mnamo mwaka 2012 ambapo ulitokea uharibifu mkubwa wa Mali, na Mifugo na serikali iliamua kutenga upya maeneo kutatua migogoro ingawa bado maeneo hayo hayakukidhi mahitaji kutokana na kutotimia kwa kiwango cha ukubwa wa maeneo kadri ilivyokubaliwa hapo awali. Baadae katibu  alisoma mapendekezo ya kuboresha changamoto hizo ambazo ni Kuanzishwa kwa Mkakati mahususi wa kuwa na kamati itakayoshughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji, kufanya sensa ya wafugaji na mifugo yao, kuwekwa na kutambulika kwa njia maalum za kupitisha mifugo, Usajili wa Wafugaji na Mifugo yao.

Aidha kwa niaba ya Chama katibu ameeleza kuwa amepata taarifa ya kitendo cha ubakaji kinachosadikika kufanywa na mtu wa jamii ya wafugaji na ametoa tamko kuwa “ Sisi kama Wafugaji tunalaani vikali na tutatoa ushirikiano ili kumbaini aliyefanya kitendo cha kinyama cha ubakaji na tunaahidi kwenda kumuona mama aliyefanyiwa kitendo hicho.”

Baada ya taarifa hiyo Mh. sawala alitoa nafasi kwa watendaji na maafisa mifugo waliohudhuria mkutano huo ambapo waliwaagiza wafugaji kuchagua mwenyekiti wa wafugaji kutoka kila kijiji agizo ambalo liliwekewa mkazo na Mkuu wa Wilaya.

Akipokea taarifa hiyo Mh. Sawala amewapongeza viongozi wa  Wafugaji kwa kuandaa na kusoma taarifa nzuri iliyojitosheleza. AIdha amejibu changamoto zote  hususani za aridhi na kuwaagiza wafugaji kuwaheshimu wakulima kwani changamoto za maeneo ya malisho na njia za mifugo zimefika mwisho “ kama alivyosema waziri kuwa atatuma timu yake kuja kupitia upya mpango wa matumizi bora ya ardhi, kwa sasa tuheshimiane ili tuishi kwa Amani. Mimi sitamuonea mtu, nitatenda haki kwa watu wote, mnatakiwa kuwaadhibu vijana wenu wanaolisha mifugo kwenye mashamba ya watu tena mnialike wakati mnatoa adhabu namimi nitakuja. Wote tunategemeana kinachotakiwa ni kuheshimiana, na tukifanya hivyo hakuna tena migogoro.” Alisema.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa