• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA CHIKICHI KUTOA AJIRA 5,000.

Posted on: May 16th, 2025

Madiwani Wilayani Rufiji Mkoani Pwani wameukubali uwekezaji wa Kilimo cha Chikichi wa hekta 20,000 unaotarajiwa kuwekezwa na Kampuni ya 'Food Star Limited' kutoka Dubai, katika Kata ya Mbwara, Chumbi na Mohoro  ili kuongeza Uzalishaji wa mafuta ya kula nchini, ambao unatarajiwaa kutoa ajira 5,000 za Moja kwa Moja na zisizo za Moja kwa Moja.

Akizungumza kwenye Baraza Maalumu la Madiwani Jana Mei 16, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri lenye lengo la kusikiliza uwekezaji huo,  Mwenyekiti wa Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanayamapori Tanzania (TAWA)  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Food Star Meja Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko, amesema uwekezaji huo wa Kilimo cha Chikichi kutasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa uagizaji wa Mafuta ya kula kutoka Nchi za nje kuja Tanzania.

Amesema Food Star Imeamua kuja kuwekeza Tanzania kwasababu ya Sera nzuri za Serikali, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan Kupitia maonyesho ya Utalii aliyoyafanya Dubai, huku akibainisha kuwa Makao Makuu ya Kampuni hiyo yatakuwa Wilayani Rufiji.

"Kampuni imeletwa kwa Shukrani kubwa ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan, kwahiyo katika maonyesho yale ya Dubai waliona Tanzania iko vipi na Wakafurahia Sera za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakaweza kuja" alisema

"Rufiji ndio itakuwa shima kubwa la Kampuni hii. Rufiji tutaipaisha kwa upande wa uwekezaji" aliongeza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Rufiji Mhe. Abdul Chobo, ametoa Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Sera nzuri za kuvutia Wawekezaji nchini, huku akisema kuwa Rufiji imeanza kunufaika na kazi nzuri ya Rais ya kuimarisha sera ya uwekezaji, huku akimshukuru Mbunge wa Rufiji na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa kwa kuwavutia Wawekezaji kuja kuwekeza Rufiji.

"Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan Kwa kuimarisha sera ya uwekezaji na leo Rufiji tumeanza kunufaika na kazi ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Maswala ya uwekezaji" alishukuru Mhe. Chobo.

"Lakini pia nichukue fursa hii kumshukuru Mbunge wetu na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa alituambia kwamba mwaka huu 2025 mpaka 2030 agenda yetu ya kwanza, kuhakikisha kwanza Rufiji tunaiinua kiuchumi na tunanyanyua maisha ya Wananchi wa Rufiji" aliongeza Mhe.Chobo.

Akiungana na Mwenyekiti wa halmashauri, Diwani wa Kata ya Chemchem Mhe. Ally Manganje alisema uwekezaji huo utasaidia kuongeza kipatoa kwa halmashauri kwa ajili ya KUTOA huduma kwa Wananchi ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA CHIKICHI KUTOA AJIRA 5,000.

    May 16, 2025
  • SIRI YA RUFIJI KUMSHUKURU RAIS SAMIA NA MBUNGE MCHENGERWA

    May 09, 2025
  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa