• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

TUENDELEE KUWAPOKEA NDUGU ZETU, AMBAO MAKAZI YAO YAMEZINGIRWA NA MAJI- DC GOWELE

Posted on: April 6th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowele amewata Wananchi kuendelea kuwapokea na kuwapa hifadhi ndugu ambao makazi yao yemezingirwa na maji na wale wanaohama maeneo ya mabondeni ili kupisha maji yaliyofunguliwa katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere, hasa katika kipindi hiki ambacho maji yanaendela kufunguliwa.

“niwaombe wale Wananchi ambao mko maeneo salama zaidi, tuwe na moyo wa kuwapokea ndugu zetu (makazi yao yalizingirwa na maji na wanaohama mabondeni), awe ndugu yako asiwe ndugu yako, mpokee na mpe hifadhi kwasababu maisha yenu ni bora zaidi” alisema Gowele.

Gowele aliyazungumza hayo jana aprili 5, 2024 wakati akizungumza na Wahanga wa mafuriko waliohifadhiwa katika Shule ya Msingi Mohoro, Kata ya Mohoro baada ya kukosa makazi, ambapo Kaya 14 zenye jumla ya Watu 67 wamepata hifadhi katika shule hiyo.

Hata hivyo Serikali Wilayani Rufiji inafanya jitihada za kutafuta maeneo mengine ya kuwahifadhi kwakuwa shule zitafunguliwa hivi karibuni.


Gowele alisema kata 12 kati ya 13 zimeathirika na mafuriko na hakuna kifo kilichosababishwa na maji yaliyofunguliwa katika mradi wa Julius Nyerere, huku akiendelea kuwashukuru Viongozi wa Kata, Vijiji, Vitongoji na Chama wanavyokuwa mstari wa mbele kutoa taarifa juu ya maeneo yao kwa serikali.

“tumekuwewa tukitoa taarifa kwa Viongozi wetu, na niwashukuru sana Viongozi hawa, kila siku tunapata taarifa katika kila kona, ili na sisi tuweze kuchukua taratibu za kiserikali na tuweze kuwasaidia ndugu zetu, na tutaendelea kutoa taarifa kupitia Viongozi hawa” alisema DC Gowele.

Hivi karibuni Kamati ya maafa ilifanya kikao na Wajumbe wa kamati za maafa wa kata zote zizilizoathirika, na kutoa maelekezo ya namna ya kufanya tathimini katika maeneo yao, ili kuisaidia serikali kupata takwimu sahihi juu ya athari zilizotokea, ambapo mpaka sasa imeshapita katika Kata zote 12 kati ya Kata 13 za Wilaya ya Rufiji.

Kwa upande wake, Mhandisi kutoka katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere Disms Mbote, amesema zoezi la kuyafungulia maji hayo lilianza toka machi 5, 2024 na litaendelea mpaka Mayi 5, 2024.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Rufiji ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mohoro, Abdul Chombo ameiomba serikali kuangalia namna ya Wanafunzi kuwaweka karibu na shule ili kuwapunguzia adha ya kuvuka mara kwa mara katika mto Rufiji.

“kama ukipatikana msaada wowote basi Wanafunzi hawa waweze kukaa karibu na shule, hata kama ikishindikana madarasa yote, basi yale ya mitihani” aliomba Mhe, Chobo.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa