• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

SERIKALI YATATUA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI RUFIJI

Posted on: August 5th, 2020

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Wiliam Lukuvi ametoa suluhisho la kudumu kwa wananchi wa Rufiji hasa wakazi wa Ikwiriri na Nyamwage ambao walikuwa na mgogoro mkubwa kati ya wakulima na wafugaji.

Katika ziara yake Mh. Waziri aliambatana na Kamishna wa Ardhi Taifa,kamishna wa Ardhi Mkoa na timu yake, Mkurugenzi kutoka Wizara ya Mifugo ,mtaalamu kutoka idara ya kilimo pamoja na wataalamu mbalimbali wa tume ya matumizi bora ya ardhi.

Akizungumza na wananchi wa nyamwage na ikwiriri aliwaambia wananchi kuwa ” Mh. Rais amenituma kuja kusikiliza kero zenu na kuzimaliza kama mlivyomuomba akiwa safarini kutoka mkoani Mtwara”

Aidha baada ya kusikilliza malalamiko ya wananchi hao juu ya migogogro ya wakulima na wafugaji, pamoja na matatizo mengine ya ardhi na makazi, ambayo yalitolewa na watu mbalimbali akiwemo ndugu, Shamte Kasim Mpita mkazi wa ikwiriri ambaye ndiye aliyemlalamikia Mh. Rais akiwa safarini  kuelekea Dar es salaam, Mh.Lukuvi ameagiza Tume yake ya wataalamu wa mpango wa matumizi bora ya ardhi kuanza kazi huku akiamuru wenyeviti wa Vijiji tisa vya ikwiriri na  nyamwage kuanza vikao na wananchi wa maeneo yao ili wao waamue matumizi ya ardhi yao bila kupangiwa na mtu. Kufuatia agizo hilo Mh. Waziri ameasisitiza kuwa mpango huo uwaangalie watu wote na hasa wanyonge, bila kubagua mfugaji au mkulima.

Mh. Waziri ameongeza kuwa amefuta hati ya umiiki wa shanba namba 2968  mwekezaji kampuni ya Safe Agriculture Products Ltd lililopo eneo la ndundu kijiji cha nyamwage ambaye ameshindwa kuliendeleza eneo hilo na kulipa fidia kwa wananchi kwa wakati aliopangiwa, na kuacha jukumu kwa wananchi kupanga upya matumizi ya eneo hilo.

Mh. Waziri ameongeza kuwa gharama za kuhakiki na kupima mipaka zitatolewa na serikali hivyo mwananchi asitoe chochote katika zoezi hilo na kumalizia kuwa ifikapo tarehe 30/10/2020 zoezi hilo liwe limekamilika na hati zitolewe kwa kila mwananchi atakayethibitika kuwa anastahili kupewa umiiki wa eneo lake pamoja na kutoa vyeti kwa vijiji na kuongeza kuwa kufanyika kwa hayo kutatoa nafasi kisheria kumshtaki yeyote atakayevunja maamuzi hayo ambayo yatasainiwa na waziri mwenye dhamana.

Katika kusikiliza maoni ya wananchi baada ya maelekezo, ndugu Shamte K. Mpita (mkazi wa ikwiriri), ndg, Asali (kiongozi wa wafugaji nywamwage), na Bi. Nuru juma ligoma , kwaniaba ya wananchi wa ikwiriri na nyamwage, wamepongeza juhudi za Mh. Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa kuchukua hatua za haraka kutatua kero zao zilizo wasumbua kwa muda mrefu. Pia wamempongeza Mkuu wa Wilaya Mh. Patrick K. Sawala na kuahidi kumpatia ushirikiano.

Akifunga mkutano huo  Mkuu wa Wilaya ya Rufiji  Mh. Patrick K. Sawala amesisitiza wanachi kuishi kwa utulivu, umoja na upendo bila kubagua mkulima au mfugaji na kutoa maelekezo kwa OCD kushughulika na wafugaji watakaochunga mifugo yao kwenye makazi ya watu na mashamba ya wakulima kwa makusudi washughulikiwe ipasavyo. Pia ameahidi kuanza ziara ya kila kata kusikiliza kero za wananchi  kuanzia tarehe 11/08/2020 siku ya jumanne katika kijiji cha nyamwage.

 

 

 

 

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa