• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

SAWALA AWASHA MOTO SUALA LA RUSHWA VIJIJINI

Posted on: February 19th, 2021


Mkuu wa Wilaya Rufiji Luteni Kanali Patrick Sawala amesema hatofumbia macho suala la baadhi ya Viongozi wa Vijiji kuumiza Wananchi kwa kujihusisha na vitendo vya Rushwa ambavyo vinapelekea kurudisha nyuma  maendeleo  Vijijini.

Ameyasema hayo wakati akitoa maelekezo kwa Watendaji kata katika kikao cha tathimini ya pili ya utekelezaji wa mkataba wa lishe ngazi ya kata Oktoba hadi Desemba 2020 kilichofanyika tarehe 19/02/2021 utete Rufiji.

Sawala amewataka Watendaji kusimamia maelekezo yanayotolewa yanayolenga kutatua changamoto za Wananchi badala ya kuwaachia Wenyeviti wa Vijiji ambao baadhi yao wanalalamikiwa sana kujihusisha na Vitendo vya Rushwa. Akiwekea mkazo kauli hiyo sawala ametoa mfano wa maeneo ambayo yanaviashiria vya Rushwa kwa kukaidi maelekezo ya serikali ya kutopokea mifugo maeneo ambayo hayajatengwa kwa malisho.

 “ kuna baadhi ya Viongozi wa Vijiji wakiwemo wa Kata ya Ikwriri wameanza kupokea mifugo kimya kimya wakati tulishaiondoa. Ikwiriri haina eneo la malisho. Hii inaashiria uwepo wa Rushwa katika maeneo hayo jambo ambalo litawapa shida Wananchi wetu. Nendeni mkasimamie vizuri maeneo hayo kwani hatutawafumbia macho Viongozi watakaobainika wanajihusisha na vitendo vya Rushwa.” Alisema

Aidha amewataka Watendaji kutumia dhamana waliyopewa kusimamia kikamilifu ujenzi wa vyumba vya madarasa na samani zake na kutaka taarifa ya utekelezaji ikamilike kufikia tarehe 23/02/2021 atakapopita kukabidhiwa vyumba hivyo. “ Hatuwezi kuzungumzia maendeleo ya Wilaya bila kuwataja Watendaji wa kata. Tumepewa dhamana hii tuitumie vizuri . mimi nitapita tarehe 23 nikute pamekamilika.” Alisema

Kwa upande wa Mifugo amehimiza kutumia kipindi hiki kuhakikisha njia za kupitisha mifugo zinajulikana na kila mwananchi, Wafugaji wanakaa kwenye maeneo yao na kuhamasisha wafugaji kutengeneza malambo katika maeneo yao yaliyotengwa ili kupata suluhisho la kudumu. “ huu ndio wakati mzuri wa kutengeneza mazingira mazuri kwa wafugaji, kuhakikisha njia za wafugaji zinatambulika ili inapofika mwezi wa saba kila kitu kipo sawa. Mfano yupo mfugaji mmoja Kata ya Chemchem amehamia eneo la Wafugaji na amekuja kuomba kibali cha kutengeneza malambo yake binafsi. Huu ni mfano wa kuigwa na ndio ufugaji wa kisasa.” Alisema

Sambamba na hayo amesisitiza suala la usimamizi wa ulipaji kodi za majengo, mabango na Vitambulisho vya ujasiriamali.

Pia ameonya suala la baadhi ya Viongozi wa Vijiji kutokaa vikao na Wananchi wao. “ Viongozi wa Vijiji wakae vikao na Wananchi wao”. Alisema

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya Bi. Maria katemana amewasisitiza Watendaji wote kuhakikisha wanatekeleza maagizo yanayotolewa kwa wakati ili kutochelewesha maendeleo ya Wananchi. “ Tuyasimamie maagizo tunayopewa ili tusicheleweshe utekelezaji.” Alisema

Naye kaimu Mkurugenzi Mtendaji Geriad Mgoba amewataka Watendaji Kata na Watendaji wote wa Serikali kutojihusisha na Vitendo vya Rushwa. “ Sifurahishwi kusikia mtendaji anahusishwa na vitendo vya Rushwa au anahusishwa PCCB kwa tuhuma za Rushwa au pato lisilo rasmi.” Alisema.

Pia amewataka Watendaji kuhakikisha wanasimamia suala la ukusanyaji wa mapato katika Vijiji vyao. “ kuna baadhi ya Vijiji havikusanyi mapato kabisa!na wengine wanahamisha mapato ya halmashauri kwenda kwenye Vijiji. Kasimamieni hilo.” Alisema

Sambamba na hilo ametoa msisitizo kwa watendaji ambao hawajakabidhi taarifa ya sehemu ya kwanza ya ukusanyaji wa taarifa za majengo kuhakikisha wanazingatia mfumo wa taarifa ulioelekezwa.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa