• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

Rufiji Yazindua Programu ya Malezi, Makuzi ya Mtoto

Posted on: December 15th, 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji imezindua programu  Jumuishi ya Taifa ya malezi na makuzi ya awali ya Mtoto yenye lengo la kutoa elimu juu ya namana ya kumlinda mtoto kuanzia mwaka 0-8 kwa ajili ya Taifa la kesho.

Uzinduzi wa program hiyo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji leo Disemba 15, 2023.

Wakichangia hoja juu ya namna bora ya kumlinda mtoto kwa mujibu wa programu hiyo baadhi ya wajumbe waliohudhuria akiwemo Ramadhani Kagea Mkazi wa Kata ya Kipugira, amedai baadhi ya Wazazi wamekuwa na tabia ya kuishi shamba huku Watoto wakiiwaacha nyumbani  peke yao Kwa lengo la kukaa karibu na Shule.

“kwa upande wangu mimi nizungumzie suala la malezi, kule ninapoishi jamii ya Watu wa kule unakuta kuna nyumba ziko Vijijini lakini kuna nyumba zipo ng’ambo ya mto ambapo ndio wanafanya shughuli za maisha za kila siku, sasa kwa kuwa Kijijini kuna nyumba na kuna Kaka yao labda wa darasa la nne au la tano ndo anabaki na wale Watoto pale Kijijini Baba, Mama wote wanakaa Shamba kwahiyo hapa maana yake Wanapata malezi ya Watoto Watupu, hamna uangalizi wale Watoto wanajilea wenyewe” amesema Kagea.

Akiunga mkono hoja hiyo na kueleza nini kifanyike Mtendaji wa dawati la Jinsia na Watoto Jeshi la Polisi Wilaya ya Rufiji INSP. Amine Iseke amesema kuna haja ya kutoa elimu na kuwataka Watoto na Walezi kutoa taarifa pindi watakapofanyiwa Vitendo vya ukatili.

“hivi vitendo vipo na ndo maana Jeshi la polisi kuna kitengo cha  Dawati la Jinsia na Watoto pia Wakaguzi Kata ambao wapo kila kata, ambao pia wanatoa hii huduma ya ulinzi na usalama na huwa Wanatoa elimu” amesema INSP Iseke.

Pia akitoa Mchango kuhusu namana bora ya kukomesha masuala ya ukatili dhidi ya Watoto Afisa Habari wa Wilaya ya Rufiji Emmanuel Kapandila ameitaka jamii kutofumbia macho na kutoa taarifa pindi wanapoona Mtoto anafanyiwa ukatili, kufanya Ufuatiliaji wa tatizo hadi mwisho ili kuhakikisha haki na wajibu vinapatikana kwa wakati .

“sisi kwenye jamii tunaweza pia tukaelimishana juu ya dhana ya kumuona mtoto wa fulani kama wa kwako, dhana hii inatakiwa kuelimishwa na kubaki katika vichwa vya jamii” amesema Kapandila.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Kibaha Yahya Mbogulume amewataka jamii Kushirikiana kwa pamoja ili kulinda usalama wa Mtoto.

“wote tuliokuwa hapa kwa Pamoja tuweze Kushirikiana tuweze kumsaidia Mtoto wa leo wa Rufiji, Watoto ndio Taifa la Kesho” amesisitiza Mbolugume.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Rufiji baada ya kuzindua program hiyo , Kaimu Katibu TawalaRichard Mwalingo ameagiza kukamatwa kwa waharifu wote watakaobainika kufanya vitendo vya Ukatili na taarifa za juu ya programu hiyo zitolewe kila mwezi kupitia ofisi ya Mkurugenzi.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa