• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

RUFIJI KUBORESHA MAKAZI YA WALIMU

Posted on: July 27th, 2022



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji John Lipesi Kayombo amefuta kilio Cha makazi duni  kwa kuahidi kujenga nyumba nne za Walimu pamoja na matundu 24 ya vyoo kwa Walimu wa Shule ya Msingi Mbwara Kata ya Mbwara ili kuboresha makazi ya Walimu pamoja na vyoo vya Wanafunzi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu.


Ameyasema hayo baada ya kuguswa na mazingira magumu ya Walimu na Wanafunzi aliyoyaona wakati alipotembelea shule hiyo Julai 24.2022 akiwa katika ziara yake ya siku tatu ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani pamoja na ruzuku toka Serikali kuu.


" Mhe. Rais anafanya kazi kubwa kuboresha miundombinu ya elimu na sekta nyingine Nchini zikiwemo nyumba za Wafanyakazi na maslahi yetu,Sisi wasaidizi wake Tutaleta fedha mapema mwezi ujao kwa ujenzi wa nyumba nne za Walimu pamoja na matundu 24 ya vyoo vya Wanafunzi kukidhi mahitaji ya shule. Tumepunguza matumizi ya ofisi na kupeleka fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo Hadi Sasa tumeshaanza miradi ya ujenzi wa Nyumba za Walimu ikiwemo shule ya Msingi Siasa, Shauri moyo na Nyakipande kwa mapato ya ndani ". Alisema Kayombo


Ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji katika utekelezaji wa vipaumbele vyake kwenye sekta ya Afya na Elimu hususani katika kutatua kero za ukosekanaji wa Jengo la mionzi, ujenzi wa Jengo hilo upo katika hatua ya umaliziaji na kuwa tayari imeshapokea mashine mpya ya mionzi ambapo huduma hiyo inatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Katika hatua nyingine akiendelea na ziara yake ya ukaguzi wa miradi Shule ya Sekondari Mohoro ameagiza kufanyika ukaguzi maalumu katika Jengo la bwalo la chakula linalotekelezwa kwa kiasi Cha shilingi milioni 100  ili kubaini matumizi ya fedha yaliyofanywa katika mradi huo.


Hata hivyo ameendelea kutoa msisitizo kwa wasimamizi wa miradi kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo kwa kuzingatia taratibu huku akizitaka kamati za ujenzi kuhakikisha zinawajibika ipasavyo na kuwa hatavumilia ikiwa kamati zitajihisisha na uhujumu wa miradi hiyo.


Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji inatekeleza miradi zaidi 152 ikiwemo miradi ya Afya na Elimu katika Kata zote 13.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • SIRI YA RUFIJI KUMSHUKURU RAIS SAMIA NA MBUNGE MCHENGERWA

    May 09, 2025
  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa