• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

RUFIJI KINARA KUKABIDHI MADAWATI PWANI

Posted on: September 1st, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mh. Luteni Kanali Patrick K. Sawala, akiongozana na Katibu Tawala Wilaya Bi. Maria Katemana, Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Rashid  Salum Salum, pamoja  na Maafisa Elimu Msingi na Sekondari wilaya ya Rufiji, leo amekabidhi madawati (viti na meza 300) kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani katika Kikosi cha Jeshi Shirika la Nyumbu Kibaha. Akizungumza katika Utangulizi wa makabidhiano hayo Mh. Sawala amesema " Tulipopewa agizo la kila wilaya kuhakikisha inamaliza tatizo la watoto kukaa chini, Rufiji tulichukua agizo hilo kuwa ni oparesheni maalumu. na tulipopata wazo toka kwako juu ya kuwashirikisha wadau likiwemo shirika la Nyumbu kwetu tulichukulia ni lazima. kwakweli wamepambana usiku na mchana mpaka kuweza kutimiza lengo na leo tunakabidhi kazi kama ulivyoagiza kuwa tar. 01/09/2020 Wilaya zote zikukabiidhi madawati kama ishara ya kumaliza tatizo la watoto kukaa chini katika Mkoa wa pwani". Wilaya ya Rufiji imefanya kazi hiyo kwa asilimia themanini(80%) kwani mpaka sasa Meza 1250 zimeshatengenezwa na viti 2031 pamoja na madawati 3945 kwa shule za msingi. Madawati haya yametengenezwa bila faida yoyote , wametoa huduma." alisema. katika kuwasilisha taarifa hiyo fupi ya Mh. Sawala amesema kazi hiyo imewajali mafundi wenyeji na kuwa mafundi wote wa Ikwiriri na Utete wamepewa kazi hiyo na tayari wameanza kukabidhi madawati hayo. Aidha amemuomba Mkuu wa Mkoa kumruhusu aanza kukabidhi madawati hayo kwenye shule zenye mahitaji ili kutekeleza kauli mbiu isemayo " Mtoto wa Rufiji kukaa chini sasa basi".

 Akiongea kwa ufupi kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Pwani amempongeza Mkuu wa Wilaya, Das, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kwa kupambana na kuwa Wilaya ya Kwanza kukamilisha na kutekeleza agizo hilo.

 Mkuu wa Mkoa Mh. Eng. Evarist Ndikilo amepongeza juhudi hizo na kusifia ubora wa madawati yaliyotengenezwa na kuwataka wakuu wa Wilaya Nyingine Kutoa maelezo ya Kina kwanini hawajatekeleza agizo lake kwa wakati.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA CHIKICHI KUTOA AJIRA 5,000.

    May 16, 2025
  • SIRI YA RUFIJI KUMSHUKURU RAIS SAMIA NA MBUNGE MCHENGERWA

    May 09, 2025
  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa