• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

REA WAKABUDHI RUNINGA KITUO VHA AFYA NGARAMBE

Posted on: November 21st, 2024

Serikali Kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamekabidhi seti ya runinga (TV) katika Kituo cha Afya Ngarambe kilichopo Kata ya Ngarambe Wilayani Rufiji, ambayo itatumika kutoa elimu kwa umàma juu ya magonjwa mbalimbali ambukizi katika jamii ikiwemo Uvico 19.

"tumekuja Kituo Cha Afya Cha Ngarambe  kukabidhi seti ya TV ambayo itatumika katika kutoa elimu kwa umma ya magonjwa ambukizi kama vile Uvico 19, magonjwa ya kuhara, pamoja na magonjwa mengine ya mfumo wa upumuaji" alisema Jayina Msuya Afisa maendeleo ya Jamii wa Wakala wa Nishati Vijijini  (REA).

Ameyasema hayo wakati akikabidhi runinga katika Kituo Cha Afya Ngarambe Jana Novemba 21, 2024.

Amesema Kituo Cha Ngarambe ni Moja ya Vituo vilivyopata umeme Kupitia mradi wa Vituo  vya Afya na pampu za maji yenye lengo la kupambana na ugonjwa wa mripuko ikiwemo Uvico 19.

"lengo la mradi huu ulikuwa ni kuwawezesha Wananchi ambao wapo maeneo ya Vijijini kupata huduma kwa haraka wanapopata athari za magonjwa hayo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ngarambe Mhe. Mohamed Ngatemela ameishukuru Serikali kwa kuendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya katika Kata yake pamoja kutoa Shukrani kwa REA kwa kutoa runinga ambayo amedai itawasaidia kutoa elimu mbalimbali ikiwemo kutoa elimu ya magonjwa yatakayokuwa yanatolewa tahadhari Kupitia vyombo vya habari.

Akizungumzia namna REA ilivyosaidia Wajawazito kupata huduma ya uzazi wakati wa usiku Mwenyekiti wa bodi ya Afya Kituoni hapo Yustina Chilowoko, amesema kuwepo kwa umeme kumekuwa msaada mkubwa  kwa Wajawazito ambapo awali walikuwa wanazalia majumbani kwa hofu ya kukutana na Wanyama Wakali gizani kutokana na kukosa umeme na kulazimika kufuata huduma hyo katika hospitali ya Wilaya kwa umbali wa zaidi ya km 60 wakipita kwenye pori lenye Wanyama Wakali.

"Tangu utufikie umeme Wajawazito wengi wanafikishwa hospitali kwa wakati na wanahudumiwa kwa wakati, hawazalii tena majumbani" Chilowoko.

Graven Kessy Muuguzi wa Kituo Cha Afya Ngarambe ameishukuru Serikali Kupitia REA kufikisha umeme Ngarambe kwasababu walikuwa wanapata shida kutoa huduma kwa Wagonjwa Nyakati za usiku.

"tunaishukuru sana REA kwa kutuletea umeme katika Kituo Cha Afya Ngarambe. Tulikuwa tunapata shida wakati wa usiku, lakini sasa  shughuli zetu zinafanyika kwa uhakika" alisema Kessy.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • MWAKILISHI WA MSAJI WA VYAMA VYA SIASA AKUTANA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA RUFIJI

    September 08, 2025
  • MSIMAMIZI WA UCHAGUZI RUFIJI AKUTANA NA VYAMA VYA SIASA KUPITIA NA KUFANYA MABADILIKO MADOGO YA KAMPENI ZA UCHAGUZI

    September 08, 2025
  • KIKAO CHA TATHMINI YA UTEKELEZAJI MKATABA WA LISHE CHAFANYIKA

    September 03, 2025
  • Camfed YAPONGEZWA KWA KUWASHIKA MKONO WANAFUNZI WA KIKE SHULENI

    August 30, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa