• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

NATOA WIKI MBILI MAENEO YOTE YALIYOTENGWA KWA AJILI YA WAFUGAJI YAENDE YAKATEMBELEWE NA KAMATI ZIJIRIDHISHE: Lt. Col. Patrick Sawala

Posted on: March 30th, 2021


Mkuu Wa Wilaya Rufiji ametoa wiki mbili kwa  Watendaji Kata kuhakikisha Wanashirikiana na Kamati za Wakulima na Wafugaji kutembelea maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya Wafugaji ili kamati hizo zenye Wakulima na Wafugaji zijiridhishe na maeneo hayo.

Ameyasema hayo jana tarehe 30/03/2021 katika kikao kazi kilichohudhuriwa na Katibu Tawala Wilaya, , Mwenyekiti wa Halmashauri, Kaimu Mkurugenzi , Kamati ya Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Wafugaji Wilaya na Kata, Wakulima na Wafugaji, Wataalam ngazi za halmashauri na Kata pamoja na Madiwani wa Kata zote,katika ukumbi wa FDC ikwiriri Wilayani Rufiji.

“Nilishatoa maelekezo kwa Watendaji kuhakikisha Vijiji vyote vinatenga maeneo na kubainisha njia za mifugo ili Wananchi wote wazijue kuepuka migogoro . sasa naongeza Wiki mbili nataka Watendaji wote mtembelee hayo maeneo pamoja na kamati zitakazoundwa na kuhakikisha wanajiridhisha kuwa  kuna malisho, na njia za kupita mifugo kuelekea kwenye maji.” Alisema

Aidha ametoa rai kwa Viongozi kuhakikisha kamati hizo zinakuwa na Wafugaji ili kuepuka malalamiko ya kutengewa maeneo yasiyofaa kwa mifugo yao.

 Pia ameagiza Mkurugenzi Mtendaji kuweka alama za vivuko kwa mifugo katika barabara , njia za mifugo toka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, kuhakikisha ngazi zote zinazopaswa kusimamia sheria zinapatiwa elimu juu ya sheria hizo.

Sambamba na hilo amepiga marufuku swala la ushushwaji wa Mifugo katika eneo lolote la Wilaya ya Rufiji, Wafugaji kuhakikisha Wanapeleka Shule Watoto wanaostahili kwenda shule, na kuunda kamati ya Wilaya ya Mifugo na Wakulima.

Kwa Upande wake Katibu Tawala Wilaya Bi. Maria Katemana ameelekeza kuhuishwa kwa kamati za vijiji za wakulima na wafugaji ili kushughulikia kwa haraka changamoto zinazojitokeza katika maeneo ya Vijiji kwa wakati. Pia amewataka Viongozi kushirikisha ngazi nyingine pindi wanapoona wanakwama katika maswala yanayohitaji ufafanuzi au uelewa. “ pale ambapo kamati zinaona zinahitaji msaada wa ngazi za juu zihakikishe zinatoa taarifa ofisi ya kata na ofisi ya kata itafanya mawasiliano kwa mujibu wa utaratibu ili kutatua. Pale ambapo tunaona tunahitaji msaada wa kisheria basi tufanye hivyohivyo na mwanasheria atatoa huduma.” Alisema.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri  Mhe. Juma Ligomba, amewataka Viongozi kuacha mara moja mambo yote yaliyosababisha kufikia hatua ya kuleta migogoro ya Wakulima na Wafugaji. “  awali kama tulikuwa hatusimamii sheria kwa makusudi twendeni sasa tukasimamie ili kupunguza migogoro isiyo yalazima”. Alisema.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa