• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

MWENYEKITI WAZAZI CCM TAIFA ASIFU UTENDAJI WA SERIKALI RUFIJI, AWATAKA KUSIMAMIA MIRADI

Posted on: January 28th, 2023



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi  na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa ndugu Fadhili Rajabu Maganya amepongeza jitihada za Serikali na Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa za kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo huku akiwataka wataalam kusimamia na kutekeleza miradi kwa wakati ili kupata matokeo tarajiwa. 


Mwenyekiti, Maganya ametoa pongezi hizo leo wakati wa ziara yake ya kwanza anayoifanya kwenye Mkoa wa Pwani kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwa pia ni maadhimisho ya kutimiza miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi.


Pamoja na wadau wengine, ndugu Maganya amemtunikia Mhe. Mchengerwa hati ya shukrani kwa kutambua mchango wake mkubwa anaoutoa katika kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Rufiji.


Aidha, ameupongeza Mkoa wa Pwani kwa kuonyesha mshikamano na ushirikiano kwenye jumuiya zote za chama katika kuwatumikia wananchi huku akiitaka mikoa yote kuiga mfano huo.



Amewataka watendaji wa Chama cha Mapinduzi katika ngazi zote nchini kuwa na nidhamu katika kusimamia fedha zote za miradi zinazotolewa na Serikali ya Chama Cha mapinduzi huku akisisitiza kuwa wao ndiyo jicho la chama katika ngazi husika.


Pia amewaelekeza kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa changamoto hizo ili wananchi waendelee kuwa na Imani na chama chao.


“Ninawapa makali ya kusimamia Ilani ya Chama cha Mapinduzi, lakini jambo la kwanza ni kusimamia kero” amesisitiza Mwenyekiti Maganya


Amewahimiza wanachama wa Chama cha Mapinduzi kukisemea chama hicho mambo makubwa ya kimaendeleo ambayo yamefanyika katika kipindi hiki kifupi chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.


Kwa upande wake, Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (MNEC) wa Mkoa wa Pwani, na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameishukuru Serikali chini ya Rais Samia kwa kutekeleza miradi mbalimbali kwa wananchi wa Rufiji.


Ametaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa kwa mafanikio makubwa katika jimbo hilo kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, vituo vya afya, shule na upatikanaji wa umeme takribani katika vijiji vyote.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa