• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

MWENGE WA UHURU WARIDHISHWA NA UKARABATI WA HOSPITALI YA WILAYA RUFIJI UTETE.

Posted on: April 5th, 2025

Mwenge wa Uhuru umeridhishwa na ukarabati wa Majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Rufiji Utete, huku Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ismail Ussi akitoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Luteni Kanali Fredrick Komba,pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Rufiji Bw. Simon Berege, kwa kusimamia vizuri ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuwadumia Wananchi.

"tumekagua na tumeona mradi, mradi huu ni wa Viwango, Mhe. Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi niwapongeze kwa kazi nzuri ya kuwahudumia Wananchi wa Rufiji. Mwenge wa Uhuru Umeridhishwa na ukarabati wa mradi huu" alisema Ussi Kiongozi wa Mbio za Mwenge.

Ussi alitoa kauli hiyo leo, Aprili 5, 2025 baada kukagua ukarabati wa hospitali ambapo Serikali ya awamu ya sita ilitoa Milioni 900 kwa ajili ya ukarabati wa majengo hayo chakavu.

Vile vile Mwenge ulizindua Bweni la Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ikwiriri pamoja na Mradi wa Maji katika Kitongoji cha Nyandakatundu Kata ya Chemchem.

Mbali na uzinduzi, uliweka jiwe la Msingi katika mradi wa Barabara ya kutoka Mahakama-kituo Cha Afya Ikwiriri kuelekea kaunda,  kutembelea Mradi wa Vijana wa kufyatua matofali Ikwiriri cha 'Vijana Taifa la Kesho', pamoja na kutembelea Mradi wa utunzaji wa Mazingira na Matumizi ya nishati safi ya Kupikia.

Ussi aliwataka Wananchi wa Rufiji kushiriki uchaguzi Mkuu octoba Mwaka huu pamoja na kuendelea kutunza amani na utulivu.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, alisema Rufiji imepiga hatua kubwa katika Kipindi cha hivi karibuni Shule zaidi 10 zimejengwa.

“Katika kipindi cha hivi karibuni, Rufiji imepiga hatua kubwa katika sekta ya miundombinu, ujenzi wa shule na vituo vya afya. Shule zaidi ya 10 zimejengwa, na vituo vya afya vimeongezeka kutoka viwili hadi kufikia tisa,” alisema Mchengerwa.

Mwenge wa Uhuru umepitia jumla ya miradi sita ya maendeleo wilayani Rufiji, yenye thamani ya shilingi bilioni 1.6. Miongoni mwa miradi hiyo ni uzinduzi wa bweni katika Shule ya Sekondari ya Ikwiriri lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80.

Kauli mbinu ya Mwenge wa Uhuru mwaka huu inasema 'Jitokezekeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 Kwa amani na Utulivu'.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • SIRI YA RUFIJI KUMSHUKURU RAIS SAMIA NA MBUNGE MCHENGERWA

    May 09, 2025
  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa