• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

'mvua ikinyesha usijifiche chini ya mti' Mwaluseke

Posted on: November 6th, 2023


Kamati ya Maafa ya Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji imeendelea kutoa elimu ya tahadhari na hatua za kuchukua dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha ili kuokoa maisha ya Wananchi.

Kutokana na utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), msimu huu kutakuwa na mvua nyingi (El-nino).

Akielezea hatua hizo Novemba 5, 2023, wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Ngorongo katika Kijiji cha Ngorongo Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Rufiji Inspekta Henry Mwaluseke, amewasihi Wananchi wasijifiche chini ya mti wakati mvua ikiendelea kuonyesha.

"Vilevile mvua ikinyesha usikae shambani rudi nyumbani, pia tukarabati nyumba zetu, kule Utete (Kitongoji cha Kiwili) nyumba tatu zimeezuliwa bati, Wananchi tusikae mabondeni tutoke huko msimu huu kutakuwa na mvua nyingi, ukiona mvua inanyesha alafu kuna radi zima kiunganishi cha umeme kwenye nyumba yako (main switch). 

Ndugu zangu huu ndio wakati wa kuonyesha umoja na mshikamano, kama tunatofauti naomba tuziache ili tuweze kusaidiana" amesisitiza Mwaluseke.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati hiyo Semeni Mbigo amezitaka Halmashauri za Vijiji kuunda timu ya dharura ya Maafa ya watu sita ili iweze kuwasaidia pindi Maafa yatakapotokea, licha ya kuwa na Kamati za Maafa katika Vijiji.

"chagueni vijana 6 wenye uwezo wa kuogelea, katika timu hiyo pia awepo Mgambo1 , skauti1, pamoja na Askari polisi Kata na Watatu waliobaki ni Wananchi kutoka kwenye Jamii zetu" amesema Mbigo.

Akiendelea kusisitiza nini Wananchi Wakifanye kipindi hiki cha mvua, Ferbet Msapila amewasistiza Wananchi kufanya usafi katika maeneo wanayoishi pamoja na kuchimba misingi ya njia za maji pembezoni mwa nyumba wanazoishi ili maji ya mvua yasiwe na uwezo wa kuangusha udongo.

Kamati hiyo mpaka sasa imeshatembelea Kata sita, Muhoro, Chumbi, Mkongo, Ngorongo, Kipugira na Mwaseni.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA CHIKICHI KUTOA AJIRA 5,000.

    May 16, 2025
  • SIRI YA RUFIJI KUMSHUKURU RAIS SAMIA NA MBUNGE MCHENGERWA

    May 09, 2025
  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa