• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

Msiweke Makazi ya Kudumu Katika Maeneo Yaliyotengwa na Serikali-DC Gowele

Posted on: January 5th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amewataka viongozi wa vitongoji na Vijiji kutoa elimu kwa Wananchi juu ya namna ya kumiliki ardhi kihalali, hali itayosaidia Wananchi kutovamia maeneo yaliyotengwa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi na kupunguza migogoro kati ya maeneo ya serikali ambayo huvamiwa na kugeuzwa kuwa makazi ya Wananchi.

Amesema imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya Wananchi kuingia katika maeneo ya serikali bila ya kujua.

Meja Gowele ametoa kauli hiyo leo January 4, 2024 wakati akizungumza na baadhi ya Wananchi wa Kitongoji cha Golani Kata ya Chemchem Wilayani Rufiji Mkoani Pwani, katika eneo la uwanja wa ndege ambapo Familia ya Mzee Saidi Matimbwa ilimuomba Mkuu wa Wilaya kwenda kurudisha eneo lao walilokuwa wanalalamika kuwa limechukuliwa ambapo baada ya Ufuatiliaji wa Nyaraka ikiwemo ramani imebainika kuwa eneo linalodaiwa limo ndani ya eneo la kiwanja cha ndege .

“Viongozi wa Vitongoji na Vijiji muwaeleze wananchi wasiweke makazi ya kudumu katika maeneo yaliyotengwa na serikali, na Mtu unapochukua eneo ni vizuri ukajua kama ni la Serikali au sio, niwaombe wanarufiji tusiweke ugumu sana kwenye maendeleo” Amesisitiza DC Gowele.

Akitoa elimu, Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Nuru Pipino amesema mtu yeyote atakayevamia na kufanya makazi katika eneo la serikali hawezi kulipwa fidia na kuwataka wananchi kuhakikisha wanafuata utaratibu pindi wanapotaka kutumia maeneo badala ya kujimilikisha nje ya utaratibu.

“serikali inalipa fidia pale tu inapoingia kwenye eneo la Mtu na huyo Mtu  awe na umiliki halali wa hilo eneo, eneo lolote likiwa linamilikiwa na taasisi ya serikali, na Mtu akaenda kuingia  kwenye lile eneo baada ya serikali kuwa na tayari inaumiliki wa hilo eneo, huyo Mtu atakuwa amevamia” amesema.

Wakikiri kuwa kuwa kiwanja chao kipo ndani ya uwanja wa ndege baada ya ushahidi wa nyaraka za kisheria Wanafamilia hiyo akiwemo Asha Muhando ameiomba serikali iwatazame kwa jicho la huruma pale walipoishi katika eneo hilo na kupanda mikorosho.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa