• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

MIRADI YA MAENDELEO YAKAGULIWA

Posted on: August 18th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji leo ameendelea kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyojengwa kwa fedha za Serikali kata za Mwaseni na Mkongo tarafa ya Mkongo na kuzungumza na wananchi wa kata ya Mwaseni kijijini Mloka mara baada ya ukaguzi wa mradi wa kituo cha afya cha Mwaseni. Kituo hicho chenye jumla ya majengo matano ambayo ni Opd, jengo la kujifungulia mama mjamzito, jengo la upasuaji, choo, jengo la kufulia, na sehemu ya kuchoma taka kimegharimu shilingi mil.400.

 Katika ukaguzi wa mradi huo mkuu wa wilaya ameagiza taarifa ya kina iandaliwe na kuhakikisha gharama inafanana na thamani ya majengo yaliyojengwa.

Baada ya ukaguzi wa majengo ya kituo cha Afya hicho Mkuu wa Wilaya amezungumza na wananchi wa Mwaseni na kusikiliza kero zao. Miongoni mwa kero ambazo wananchi wamemuomba Mkuu wa Wilaya kuzitatua ni pamoja na swala la kituo cha Afya kuchelewa kutoa huduma kwa wananchi, tembo na nguruwe pori  kuharibu mazao mashambani,ukosefu wa fursa za kufanya kazi kwenye mradi wa bwawa la umeme la Mwl. Nyerere, gari la kubebea wagonjwa kuwa bovu  pamoja na kero ya ng’ombe kuingia katika mashamba na kula mazao.

Akijibu kero hizo Mkuu wa Wilaya aliwajibu wananchi kuwa kituo cha Afya kitaanza kazi hivi karibuni na kueleza kuwa daktari tayari ameshaandaliwa ambaye ni mtaalamu wa upasuaji na magonjwa mengine.Katika swala la wanyama kuingia mashambani Mkuu wa Wilaya ameahidi kuonana na wataalam wa TANAPA ili kujadiliana namna ya kutatua changamoto hiyo. Pia kwa swala la ukosefu wa fursa za mradi Mh. Sawala amewataka viongozi kuwapa kipaumbele vijana wa mwaseni na Rufiji kwa ujumla ndipo wapate vijana wengine kama utaratibu unavyotaka. Vilevile kwa upande wa kero ya ubovu wa gari la wagonjwa Mh. Sawala amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji kushughulikia matengenezo ya gari hilo.

Akifunga mkutano huo, Mkuu wa wilaya alihamasisha jamii juu ya swala la elimu, kulinda Amani na usalama wao wakati wa kampeni kwa kutojihusisha na vurugu za  kisiasa na kuwa watoe taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji juu ya mgeni anayeingia katika kitongoji.

Katika tukio lingine, Mkuu wa Wilaya alitembelea mradi wa zahanati ya Mkongo illiyogharimu shilingi Mil.200 ambapo jengo la opd limegharimu mil.175 na choo mil.25 mradi upo katika hatua za mwisho na unatarajiwa kuanza tar. 30 mwezi huu.

Pia amekagua mradi wa mabweni mawili na madarasa mawili mradi ambao umegharimu jumla ya shilingi mil. 190. Mil.150 zikiwa ni kwaajili ya mabweni mawili na mil.40 madarasa mawili. Vilevile amekagua ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Ruwe mradi uliofadhiliwa na TEA( MAMLAKA YA ELIMU T amabao Umegharimu shilingi mil.95. mil. 60 ikiwa ni gharama za vyumba vitatu vya madarasa na samani zake na mili.35 zimetumika kujenga matundu 24 kwaajili ya vyoo.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa