• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

Miradi 8 yazinduliwa, 1 wakataliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Wilayani Rufiji

Posted on: July 13th, 2018

Wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2018 wakiongozwa na kiongozi wao Ndugu Charles Francis Kabeho wametembelea jumla ya miradi 9 ya Maendeleo Wilayani Rufiji.

Miradi hiyo ni ya maji safi na salama, elimu, afya, kiwanda cha kutengeneza samani, nyuki, kilimo cha korosho, na ujenzi wa miundombinu ya barabara ya lami. Miradi hiyo yenye thamani ya kiasi cha Shilingi za Tanzania 2,564,489,040.00/= imefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali, wahisani na wajasiliamali.

Mradi wa uchimbaji na ujenzi wa kisima cha maji shule ya Msingi Umwe uliogharimu kiasi cha Sh. 6,000,000/= ulidhaminiwa na Taasisi ya Al firdaus Charitable Foundation Sh. 5,000,000/=, Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Sh. 600,000/= na nguvu za wananchi Sh. 400,000/=. Akisoma taarifa ya mradi, Mtendaji wa kijiji cha Umwe Kaskazini amesema kuwa kisima hicho kitasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wanafunzi, walimu na jamii nzima inayoizunguka shule ya Msingi Umwe. Mara tu baada ya uzinduzi wa kisima hicho Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Ndugu Charles Francis Kabeho amewaasa watumiaji wa chanzo hicho cha maji kuwa makini na kukitunza ili kiweze kudumu kwa muda mrefu.

Ujenzi wa kituo cha Doha Kheri kijiji cha Umwe Kaskazini uliogharimu Sh. 380,000,000/= fedha iliyotolewa na wahisani Al ATA’A Charitable Foundation na eneo lilitolewa na mwananchi ndugu Mohamed Selemani Mohamed. Kituo hicho kimejengwa kwa ajili ya wananchi wanaoishi katika mazingira hatarishi na utaratibu wa kujenga vyumba vya madarasa ili watoto waweze kupata elimu unaendelea. Akiongea mara tu baada ya kukagua miundo mbinu hiyo ya Doha Keri, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 ndugu Charles Francis Kabeho amepongeza jitihada zinazofanywa na uongozi wa kijiji cha Umwe Kaskazini kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuhakikisha kuwa wananchi wanapata Maendeleo. Hata hivyo kiongozi huyo amewaagiza viongozi wa kijiji kuhakikisha unafanya utaratibu wa kupata hati ya kisheria ya umiliki wa ardhi hiyo.

Ujenzi wa uboreshaji wa kituo cha Afya Ikwiriri wenye thamani ya Sh. 404,815,240/=  kati ya hizo fedha za Serikali Sh. 400,000,000/=, Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Sh. 1,200,000/= na nguvu kazi ya wananchi Sh. 3,615,240/= umekataliwa kuwekewa jiwe la Msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 kutokana na taarifa za fedha kutofautiana. Taarifa ya mkoa inaeleza mchango wa nguvu za wananchi ni Sh. 1,000,000/= wakati taarifa iliyosomwa na Mganga Mfawidhi Dr.. IDD RAJAB MALINDA wa kituo cha Afya Ikwiriri ni Sh. 3,615,240/=. Hivyo kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 amemwagiza Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya kufuatilia sababu za kutofautiana kwa takwimu hizo za fedha.

Mradi wa kikundi cha Useremala Mkongoni wenye thamani ya Sh. 20,000,000/= nao umetemebelewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018.Baada ya kupokea zawadi mbalimbali zinazotokana na zao la misitu, ndugu Charles Francis Kabeho amewashukuru wanakikundi na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kumuunga mkono Mh. Dr. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania ya kutengeneza Tanzania ya viwanda. Hata hivyo kikundi hicho kimeaswa kuchapa kazi kwa bidii na weledi wa hali ya juu.

Miradi mingine iliyotembelewa na Kiongozi wa mbio za mwenge ni pamoja na RahmaKheri Village wenye thamani ya Sh. 1,093,940,500/=. Mradi upo kijiji cha Chumbi C na umedhaminiwa na African Relief Organization. Lengo kuu la mradi huu ni kuwasaidia wananchi wasiojiweza kwa kuwapatia huduma muhimu ambazo ni makazi, zahanati, shule na msikiti. 

Mradi wa Nyuki wenye thamani ya Sh. 11,903,000/= katika kijiji cha Mohoro. Lengo la kuanzisha mradi huu ni pamoja na kuhamasisha uhifadhi wa misitu, upatikanaji wa makundi ya nyuki, upatikanaji wa asali na kutoa elimu ya ufugaji nyuki kwa jamii. 

Shamba la mikorosho lenye thamani ya Sh. 34,850,000/= la mkulima kijiji cha Nyamwage ambaye pia ni Mh. Diwani wa Kata ya Mbwara Bwn: Juma A. Ligomba. Akisoma taarifa yake mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018; mkulima huyo ameiomba Serikali kuongeza kiwango cha mikopo kwa vijana ili waweze kuwekeza katika miradi mbalimbali kwa lengo la kujiongezea vipato vyao. Aidha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amempongeza mkulima huyo kwa kuwa mfano kuigwa katika jitihada za kupambana na umaskini kwa kuanzisha mradi wa kilimo cha zao la korosho na kuwaasa wananchi wengine kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo binafsi na Taifa kwa ujumla.

Ujenzi wa madarasa 4 na ofisi 1 ya walimu katika Shule ya Sekondari Utete wenye thamani ya Sh. 80,000,000/=.  Katika ziara hiyo pia Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amewatunuku vyeti wanafunzi 4 waliofanya vizuri kimasomo kwa mwaka 2017.  Akiongea mara baada ya uzinduzi wa madarasa hayo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Utete Bwn: Hillary Bassa Ngela amesema kuwa upatikanaji wa madarasa hayo utatua kwa kiasi kikubwa uhaba wa madarasa uliokuwa unaikabili shule hiyo na hivyo kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza. 

Ujenzi wa barabara ya Bomani – Mbuyuni (0.65km) kwa kiwango cha lami wenye thamani ya Sh. 535,595,540/=. Akisoma taarifa ya mradi mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018, Meneja wa TARURA Eng. Sambo G. Mahona amesema kuwa kuanzishwa kwa mradi huo ni hatua ya kuboresha mji wa Utete ambao ni makao makuu ya Wilaya ya Rufiji na utakuwa ni mwendelezo wa mpango wa Wilaya wa kuhakikisha barabara zote muhimu katika mji wa Utete zinajengwa katika kiwango cha lami.






Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa