• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

MH. SAWALA: MBWARA SISI NI WATUMISHI WENU, MTUTUME.

Posted on: September 3rd, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji,M, Mh. Luteni Kanali Patrick K Sawala amewataka wanakijiji  wa kijiji cha Mbwara kutumia viongozi wao kusema mahitaji yao ili watekelezewe kwa wakati badala ya kukaa kimya. “ Sisi viongozi wenu ni watumishi wenu. Mtutume.” Ameyasema hayo  leo alipokuwa kwenye Mkutano na Wanakijiji cha Mbwara kata ya Mbwara ikiwa ni katika kutekeleza ahadi yake ya kuzunguka kata zote na vijiji vyote kushughulikia kero za Wananchi wa Wilaya ya Rufiji. Akizungumza katika utangulizi wa kikao hicho Mh. Sawala alisema “Mimi nimekuja kushirikiana na watu wa Mbwara, peke yangu siwezi. Maendeleo ya Mbwara yanaletwa na Wana Mbwara wenyewe. Semeni mahitaji yenu nami nitayafanyia kazi”.

Baada ya Utangulizi huo Mh. Sawala aliwaruhusu wananchi kuanza kutoa kero zao ambapo Bw. Saidi Kipengele alilalamikia tatizo la ubovu wa miundombinu ya maji hasa kupasuka kwa mabomba na ubovu wa jenereta inayotumika kuzalisha umeme wa kuendesha mitambo ya maji. Bw. Sefu A. Kingwande amezungumzia swala la Elimu hususani upungufu wa Walimu katika Shule ya Msingi Mbwara ambayo inawananfunzi takribani 466 na walimu 04 tu. Pia Bi. Tabia Kibure ameomba msaada wa kuungwa mkono katika uchangiaji wa madawati Shule ya Sekondari Mbwara. Kero nyingine ni pamoja na upungufu wa wahudumu katika zahanati, Wizi wa kuku na pikipiki, kutojulikana kwa mipaka ya kijiji cha Mbwara na Kitapi, pamoja na Mbwara na Tawi.

Akijibu kero hizo Mh. Sawala amesema tatizo la maji lilikuwa ni uzembe wa wasimamizi kwa kushindwa kutoa fedha ya mafuta wakati maji yalikuwa yanalipiwa na wanakijiji, “ Ninatoa maelekezo. leo jioni nipate taarifa kuwa Jenereta linawaka. Haiwezekani jenereta halijawashwa miaka na miaka. Huo ni uharibifu wa mali za Serikali. Nataka tatizo la maji liishe.” Akiongezea katika kujibu kero ya maji Meneja wa Tanesco Ndg. Said M. Masoud amesema wameshaomba Transifoma kwaajili ya kuunganisha umeme kwenye mradi wa maji hivyo ikiletwa muda wowote litafungwa na mitambo itaanza kutumia umeme wa vijijini. Katika suala la Elimu na Madwadi ameahidi kulifanyia kazi mara moja na kuwa madawati ndani ya wiki mbili yatakuwa yamepatikana. Pia katika suala la Wizi Mh. Sawala amewataka wanakijiji kuwa na mpango wa ulinzi shirikishi na kutoa ushirikiano kwa polisi ili kubaini wahalifu na kuwakamata sambamba na hilo, ametoa maelekezo kwa wananchi kuwa kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake na kutoa taarifa kwa viongozi pindi wanapomuona mtu mgeni katika mazingira yao. kwa upande wa upungufu wa wahudumu wa Afya na dawa Mh. Mkuu wa Wilaya kupitia Mganga Mkuu wa Wilaya ameasema tayari maombi ya watumishi 17 yameshafanyika ili kuziba mapengo ya watumishi katika vituo na zahanati na kuwa kwa zahanati iliyokuwa imekosa usajili MSD imeshashughulikiwa na ndani ya wiki mbili usajili utakuwa umekamilika. Vilevile amejibu tatizo la Migogoro ya mipaka ya vijiji kwa kuwataka wanakijiji kuwa watulivu wakati timu ya mipango ya udhibiti wa matumizi bora ya ardhi inaendelea.

Akifunga Mkutano huo Mh. Sawala amewataka wananchi kufanya kampeni za kistaarabu na kuepuka kujihusisha na vitendo vya vurugu.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA CHIKICHI KUTOA AJIRA 5,000.

    May 16, 2025
  • SIRI YA RUFIJI KUMSHUKURU RAIS SAMIA NA MBUNGE MCHENGERWA

    May 09, 2025
  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa