• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

MCHENGERWA AWAKIMBILIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO RUFIJI, ATOA MILIONI 40

Posted on: April 3rd, 2024

Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamedi Mchengerwa, ametoa pole kwa Wananchi wa Rufiji ambao mazao yao yameathirika kwa maji yaliyofunguliwa katika mradi wa kuzalisha umeme wa bwawa la Julius Nyerere, baada ya bwawa hilo kujaa kupita kiwango kilichokusudiwa, hali iliyosababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha.

Mchengerwa ametoa pole hizo jana Aprili 2, 2024 wakati akizingumza kwa nyakati tofauti na Wananchi wa Nyamwage, Chumbi, Mohoro na Utete, ikiwa ni ziara yake ya kuwapa pole Wananchi wa Rufiji.


“poleni sana kwa kupoteza kila kitu” alisema Waziri Mchengerwa.

Mbali na hayo, Waziri Mchengerwa ameahidi kutoa fedha kiasi cha shilingi  milioni arobaini kwa Wananchi walioathirika ili isaidie kununua mbegu zitakazopandwa baada ya kipindi cha kufunguliwa maji hayo kupita.

 “kila mwaka huwa tunakuwa na shughuli ya kufuturisha, lakini kwa mwaka huu kutokana na mafuriko haya, kile kiwango cha mshahara wangu na nimedunduliza kidogokidogo, nikasema leo nije hapa (kutoa pole), fedha niliyotenga kwa ajili ya kufuturisha ilikuwa milioni 40, sasa nitaikabidhi ili kumwezesha kila Mwananchi wa Rufiji apate mbegu” aliongeza Mchengerwa


Akitoa taarifa fupi, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele alisema hakuna kifo kilichotokana na mafuriko hayo, na kuongeza kuwa Kamati ya maafa inaendelea kufanya tathimini ya namna Wananchi walivyoathrikia, ambapo mpaka sasa imeshafanyika katika kata 6.

Waziri Mchengerwa amesema kuwa amefarajika kuwaona Wananchi wa Rufiji namna walivyokuwa pamoja wakishirikiana na viongozi wa Serikali baada ya maafa hayo kutokea na kusisitiza kuendelea kushikamana na Serikali ili kukamilisha ndoto za mafanikio katika Wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine, Mchengerwa aliwataka Viongozi wa Serikali Nchini kushikamana pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.

Vilevile Mchengerwa aliwataka Wazazi kuwasisitiza Watoto wao wasome kwa bidii ili waje kuisaidie jamii inayowazunguka.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa