• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

MCHENGERWA AMTAKA MKANDARASI WA DARAJA LA MBAMBE KUONGEZA KASI YA UJENZI

Posted on: March 17th, 2025

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa, amemtaka mkandarasi Kampuni ya Nyanza Road Works kuongeza kasi ya ujenzi wa Daraja la Mbambe lenye urefu wa meta 81 linalounganisha Barabara ya Ikwiriri - Mloka, ili likamilike kwa wakati na kuondoa adha ambayo wananchi wilayani Rufiji wamekuwa wakikabiliana nayo.


Waziri Mchengerwa ametoa maelekezo hayo kwa mkandarasi huyo, wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kuhimiza ukamilishaji wa ujenzi wa daraja hilo la Mbambe linalojengwa katika Kijiji cha Mbambe, Kata ya Mkongo wilayani Rufiji.

“Mkandarasi ongeza kasi ya ujenzi wa daraja hili kwani asilimia 22 iliyofikiwa bado ni ndogo sana, na kwa kasi hii ndogo mnayoenda nayo mvua zikiongezeka zitaleta changamoto itakayokwamisha ujenzi wa daraja hili,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

“Mkuu wa Wilaya naelekeza Meneja wa TANROADS mkoa kuanzia wiki ijayo aje kuwalipa fidia wale wote waliohakikiwa madai yao, kwani Rais Samia amekwishatoa fedha milioni 500 kwa ajili ya fidia,” Mhe. Mchengerwa ameelekeza.

Mchengerwa aliyazungumza hayo Jana Machi 17, 2025 wakati akiwa njiani kuelekea Kijiji Cha Kilimani kupata futari pamoja na Wananchi.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Mradi upande wa Mkandarasi Kampuni ya Nyanza Road Works Mhandisi Emmanurel Owoya amesema kuwa, ujenzi wa daraja umefikia asilimia 22 ampapo tayari nguzo za msingi 64 zimeshajengwa kati ya 107 zinazotakiwa kujengwa, na juu ya hizo

 nguzo litamwagwa zege ikiwa ni pamoja na kujenga makalavati makubwa 3 na dogo moja.

"daraja lina meta 81,lakini pia Kuna madaraja madogo madogo Manne, yapo makubwa matatu yana milango minne ya Mita tano tano (upana Mita 5 na kwenda juu Mita 5). Lakini pia Kuna daraja dogo lenye Karavati Moja, lakini pia tutajenga kilometa 3 za maingilio kwa kiwango cha lami, kiujumla tupo kama katika asilimia 22 hivi za utekelezaji, kwahiyo hiyo ndio kazi ambayo tutaifanya hapa kwenye mradi" alifafanua Eng. Owoya.

Jumla ya Shilingi bilioni 24, 164, 904, 622 zitatumika kujenga daraja la MBAMBE lenye urefu wa meta 81 ikijumuisha ujenzi wa barabara za maingilio kilomita 3 pande zote mbili za daraja kwa kiwango Cha lami.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA AMWAGA BIL. 50 BARABARA YA IKWIRIRI -MKONGO

    June 23, 2025
  • DC KOMBA AAGIZA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI ITOLEWE KWA KATA ZOTE RUFIJI.

    June 26, 2025
  • WATUMISHI WA UMMA RUFIJI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI, WASISITIZWA KUFANYAKAZI KWA BIDII, WAONYWA KUTOA HUDUMA KWA UPENDELEO MAOFISNI

    June 25, 2025
  • BEREGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA MKONGO, KIPUGIRA, NGORONGO

    June 11, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa