• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

MAWAZIRI 5 WA KISEKTA WAFANYA ZIARA YA KUONA MAFURIKO RUFIJI.

Posted on: April 10th, 2024

Mawaziri watano, wa Kisekta wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (sera, bunge na uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, wamefanya ziara Wilayani Rufiji kwa ajili ya kutoa pole na kujionea hali halisi ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Kamati hiyo ya maafa ya Kitaifa imefanya ziara hiyo jana Aprili 10, 2024 na kuzungumza na Wananchi katika Kijiji cha Mohoro Mashariki Kata ya Mohoro, ambapo Mhagama alisema mafuriko ya mwaka huu yalitabiriwa na Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA),  toka mwaka jana kuwa nchi yetu itapata mvua za el-nino zitakazoungana na mvua za masika na vuli.

“tunachotakiwa kufanya ni kusikiliza maelekezo ya Serikali” alisema Mhe. Mhagama.

Mhe. Mhagama amesema serikali imeshaleta tani 40 za Mahindi huku tani za unga wa Mahindi, tani za maharage na mafuta ya kupikia zikiwa zipo njiani, na kwamba serikali inaandaa tani zaidi za Chakula na madawa ili kuhakikisha Wananchi wanakuwa salama.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele, amesema”tuliweza kutoa taarifa mapema na tuliwahamisha Wananchi maeneo ya mabondeni, ndo maana tumeweza kupunguza athari za vifo. Tunamshukuru Mhe. Rais tumeweza kupokea shehena ya vyakula, mahema, na tumeweza kupata madawa ambayo yanaenda kuwasaidia ndugu zetu wasipate magonjwa ya mripuko ” alisema Gowele.

Pia Gowele aliongeza kuwa “lakini pia tunao mpango makakati ambao tayari tumeshauanza wa kuwapa maeneo (wanaokaa maeneo ya mabondeni), tayari katika kijiji cha Mohoro tuna zaidi ya Viwanja 600 ambavyo tushavitenga na tulishawagawia baadhi ya Wananchi” aliongeza Gowele.

Mawaziri wengine waliokuwa katika ziara hiyo ni Waziri wa Ulinzi Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanwake na Mkundi Maalumu Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa na Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso.

Manaibu Waziri Waliokuwa katika msafara huo ni Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Joyce Kapinga, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula, Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Godfrey Kasekenya na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sirro.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa