• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

MADIWANI WASHAURI SERIKALI ZA VIJIJI ZIONGEZEWE NGUVU KUKABILIANA NA WAFUGAJI WAVAMIZI.

Posted on: February 19th, 2024

Siku chache baada ya Mkuu wa Wilaya ya Rufiji kufanya Mkutano wa Wakulima na Wafugaji Katika kata ya Umwe- Ikwiriri Februari 9, 2024 wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero zao, Madiwani Wilayani Rufiji wameomba serikali za vijiji ziongezewe nguvu pale wanapoomba msaada juu ya matatizo ya Wakulima na Wafugaji ili waweze kusaidiwa kwa haraka ili kupunguza migogoro.

Ombi hilo liliwasilishwa leo Februari 19, 2024 na Diwani wa Kata ya Mbwara Mhe. Juma Ligomba katika kikao cha kuwasilisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya Kata kwa robo ya pili ya mwaka 2023/ 24 uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji.

Amesema licha ya kazi kubwa inayofanywa na Kamati ya ulinzi na usalama wa kuhakikisha wanadhibiti tatizo hilo pia kuna haja ya kutoa msaada wa haraka kwa serikali ya Vijiji pale wanapohitaji masaada kutoka kwa kamati hiyo.

 “Mheshimiwa Mwenyekiti changamoto hii imeshakuwa kubwa sana, tunafahamu Mkuu wa Wilaya anafanyakazi kubwa na kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha wanawaondoa Wafugaji wanaoingia katika mashamba ya Wakulima.

“naomba Mheshimiwa Mwenyekiti tuangalie namna ya kuzisaidia serikali zetu za vijiji ili inapotokea changamoto (kwa maana ya kuomba msaada wowote inapotokea) waweze kusaidiwa ili kumaliza tatizo” alisema.

Katika kikao cha Wakulima na Wafugaji Februari 9, 2024 Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele alisema ameunda vikosi kazi vinne kwa ajili ya kukabiliana na tatizo hilo.

Alisema ameunda vikosi katika ukanda wa Mwaseni, Ikwiriri, Muhoro na Utete.

Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Mhe. Abdul Chobo amesema kama Madiwani waliidhinisha bajeti kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo hivyo wataendelea Kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

“sisi Waheshimiwa Madiwani bajeti hii ambayo tunakwenda nayo ya mwaka 2023/24 tuliidhinisha kifungu cha fedha kwa ajili ya kukabiliana na jambo hilo, nilihakikishie baraza  tutaendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama na kufuatilia kule ambako kuna changamoto kubwa tuongeze nguvu ili kuweza kuhakikisha ulinzi na usalama. Lakini pia hata mwaka huu tumetoka kupitisha bajeti na suala hilo tumelizingatia”.amesema Abdul Chobo.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • BEREGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA MKONGO, KIPUGIRA, NGORONGO

    June 11, 2025
  • BEREGE AKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA MOHORO.

    May 29, 2025
  • WAKUSANYA KODI RUFIJI WAPEWA MAFUNZO UKUSANYAJI WA KODI YA MAJENGO, PANGO LA ARDHI NA USHURU WA MABANGO.

    May 26, 2025
  • BEREGE AWATAKA WAFANYABIASHARA RUFIJI KUANZA KUJIANDAA NA KUZITUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI

    May 21, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa