• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

MADIWANI RUFIJI WAELEZA WALICHOJIFUNZA BAADA YA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MAAFA

Posted on: June 27th, 2024

Mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Idara ya Menejimenti ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu kwa Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Rufiji yamehitimishwa jana Juni 27, 2024, yaliyolenga kuwajengea uwezo wa kuratibu maswala ya Maafa kuanzia jinsi ya kuzuia, kujiandaa na Maafa, Kukabiliana nayo yatakapotokea Maafa na jinsi ya kurejesha hali baada ya Maafa, huku baadhi ya Washiriki katika mafunzo hayo wakiwemo Madiwani wameishukuru Serikali kwa namna walivyoandaa mafunzo kwa Kamati ya Maafa Rufiji.

Mafunzo hayo yaliyokuwa yanaendeshwa na Wakufunzi mbalimbali akiwemo Dr. Christopher Mzava ambaye ni mshauri wa maswala ya Maafa,  amesema Wamekuja Rufiji kutoa mafunzo kwa ajili ya usimamizi wa maafa kwa Kmati ya Maafa ya Wilaya ya Rufiji, ili kuhakikisha kuwa Kamati hiyo inakuwa na uwezo wa kuratibu maafa.

“tumekuja hapa Rufiji kutoa Mafunzo kwa ajili ya usimamizi wa Maafa kwa Kamati ya Maafa ya Rufiji, wa maana ya Kamati elekezi na Wataalamu wa halmashauri, lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba timu hizi zinakuwa na uwezo wa kuratibu maswala ya maafa kuanzia kuzuia, kujiandaa, kukabiliana na hata kurejesha hali wakati Maafa yanapokuwa yametokea” alisema Dr. Christopher Mzava.

Akifunga Mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele, ameishuru Serikali kwa kuleta mafunzo kwa Kmati ya Maafa ya Wilaya ambayo yametoa mwanga ya namna ya kuratibu pindi yatakapotokea Maafa.

Sasa kila mmoja ameona element yake ni ipi na anatakiwa afanye nini, kama ni Mtu wa uokoaji, Mtu wa Medical kama ni Mtu wa usafirishaji ameshaona nini anatakiwa afanye, na hayo tutaendelea kuyafanya pale tutakapopata muda” alisema DC Gowele alipokuwa anaelezea jinsi alivyoona mafunzo kwa vitendo ya jinsi gani ya kufanya kuzuia, kujiandaa na maafa, kukabilina nayo na jinsi kurejesha hali baada ya Maafa.

Elimu ya Mafunzo hayo yalikuwa yanafanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuanzia Jumatatu Juni 24, 2024, Akielezea kitu alichojifunza Diwani wa Kata ya Mbwara Juma Ligomba, amesema amejifunza muundo mzuri wa jinsi gani ya kukabiliana na maafa ikiwemo, jinsi ya kuzuia, kujiandaa na maafa, kukabiliana nayo pamoja na kurejesha hali baada ya maafa kutokea katika jamii.

“muundo ule ambao leo mmenielekeza, nafikiria nikirudi kwenye Kata yangu nikafanye mafunzo kama ambayo mimi nimeyapata, ili Wananchi wangu wabaki wakiwa salama” alisema Mhe. Ligomba.

Diwani Mwingine, Zainabu Mng’ombe amesema amejifunza mpangilio mzuri wa utoaji wa taarifa wakati wa Maafa, “nimejifunza protocal za utoaji wa taarifa, huko mwanzo siku najua nilikuwa nafikiria kwamba hata mimi Diwani endapo nitajua kuna jambo limetokea naweza nikatoa taarifa, naweza nikasismama na nikasema, kumbe taratibu za kisheria haziko hivyo yupo Msemaji ambaye ni DC” alisema Mhe. Mng’ombe.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA AMWAGA BIL. 50 BARABARA YA IKWIRIRI -MKONGO

    June 23, 2025
  • DC KOMBA AAGIZA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI ITOLEWE KWA KATA ZOTE RUFIJI.

    June 26, 2025
  • WATUMISHI WA UMMA RUFIJI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI, WASISITIZWA KUFANYAKAZI KWA BIDII, WAONYWA KUTOA HUDUMA KWA UPENDELEO MAOFISNI

    June 25, 2025
  • BEREGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA MKONGO, KIPUGIRA, NGORONGO

    June 11, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa