• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

LISHE BORA NI MSINGI WA UCHUMI, AFYA NA USTAWI WA JAMII BORA:

Posted on: October 16th, 2020


Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Patrick Sawala, amewataka wajumbe wa
kakao cha tathmini ya kwanza ya mkataba wa Lishe ngazi ya kata julai - septemba 2020 ambao ni Mkurugenzi Mtendaji , Watendaji wa kata na Wataalamu wa Afya Wilaya, kujadili kwa kina kuona Mafanikio na madhaifu katika utekelezaji wa Mkataba huo ili kuweza kujipanga vyema katika kuboresha na kutekeleza mkataba huo kwa asilimia miamoja.

Mratibu wa Lishe Wilaya Bi. Mwanahamisi Lyana aliwasilisha taarifa ya hali ya Lishe kitaifa, Kimkoa na ngazi ya Wilaya ambapo kwa Wilaya mpaka kufikia juni 2020 Uzito pungufu ni asilimia 8.3, Upungufu wa damu kwa mama wajawazito asilimia1.3, Ukondefu asilimia 0.54 na Udumavu asilimia 0.1. akisisitiza juu ya umuhimu wa Lishe, Mwanahamisi alisema " ndani ya siku 1000 kuanzia ujauzito ni kipindi madhubuti Cha kuweka mkazo ili kupata kizazi kilichobora".

Naye Afisa Lishe Bw. Omary Kombo aliwasilisha taarifa ya Kadi alama ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe ngazi ya Kata na Vijiji na ambapo ilionekana kuwa Kata ya Chemchem ina asilimia 0.5 ya Watoto wenye utapiamlo, Ngarambe asilimia 1, Umwe asilimia 12, na Utete asilimia 4.

Wakijadili uboreshaji wa Elimu ya Lishe na Ufuatiliaji ili kuhakikisha Wilaya haipati Watoto wenye Utapiamlo wajumbe wamekubaliana kuhakikisha Sheria ndogo zinawekwa na kusimamiwa ngazi ya Vijiji na Vitongoji, Kila Kijiji na Kitongoji kufanya maadhimisho ya ya siku ya Lishe ili kuongeza mwamko na elimu ya Lishe kwa Umma, Kubandika mmatangazo ya huduma za Lishe katika mbao za matangazo kwenye Ofisi za kata na Vijiji, Kuwawezesha Watendaji wanaotoa huduma za Afya ya jamii vijijini ili kuweza kufikia Wananchi kwa urahisi na kwa Wakati, na kuwasilisha taarifa za kila robo.
Akitoa msisitizo kwa Watendaji, Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Ally Zuberi Mbikilwa ameomba Viongozi kufuatilia kwa Ukaribu hasa kwenye swala la uandaaji wa taarifa ili zipatikane kwa wakati ," Rufiji tunakila kitu, ni aibu kuwa na Watoto wenye Utapiamlo".

Aidha Mhe. Sawala amewataka Watendaji wa Kata kusimamia na kutoa Elimu kwa Watumishi kutumia lugha nzuri wanapotoa huduma kwa Wananchi na zaidi kutoa taarifa zenye kuridhisha kwa Wananchi hasa kwenye Swala la dawa. " Wahudumu wa Afya watoe Elimu kwa Wananchi pindi inapotokea dawa zinazohitajika haziruhusiwi kutolewa kutokana na kiwango cha zahanati. Wazee wengi wanalalamika kukosa dawa kumbe dawa zao zinatolewa kwa kiwango cha hospitali ya Wilaya au pengine Kituo cha Afya lakini utashangaa Wahudumu wanasema tu dawa hakuna." Alisema.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • SIRI YA RUFIJI KUMSHUKURU RAIS SAMIA NA MBUNGE MCHENGERWA

    May 09, 2025
  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa