• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

KILA MMOJA AWE MLINZI WA MIRADI YA MAJI- WAZIRI AWESO

Posted on: January 27th, 2024


Waziri wa Maji Juma Aweso, amewataka Wananchi wa Rufiji Mkoani Pwani kuilinda na kuitunza miradi ya Maji inayotekelezwa katika maeneo yao kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae.

Waziri Aweso amesema wapo baadhi ya Watu wasiopenda maendeleo wamekuwa wakiharibu miundombinu kwa kuvunja mabomba ya Maji

"tumeshuhudia baadhi ya maeneo, tunajenga mradi, Watu walikuwa na shida ya Maji, lakini wakati mwingine mtu akigombana na mkewe hasira zake anakuja kuvunja bomba la Maji. Sasa kila mmoja awe mlinzi kwa mwenzake, kuhakikisha mradi huu ambao Rais ameweka fedha nyingi unakuwa na faida ya vizazi vya sasa na baadae" amesisitiza Waziri Awesu

Awesu ameyazungumza hayo Januari 27, 2024  kwenye mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kijiji cha Chumbi A, Kata ya Chumbi Wilayani Rufiji, alipokwenda kuzindua mradi wa Maji wenye thamani ya shilingi Ml. 722 ambao utahudumia Wakazi 8664 wa Kata ya Chumbi.

Kwaupande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amempongeza Waziri huyo kwa kufika Chumbi na kuzindua mradi huo ambao utasaidia kuwapunguzia adha Wananchi ya kwenda kutafuta Maji umbali mrefu.

Katika hatua nyingine, akizungumza kwa niamba ya Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri amemuomba Waziri wa Maji kuanzisha Mamlaka ya Maji taka katika Mkoa wa Pwani.

"sisi Mkoa wa Pwani hatuna Mamalaka za Maji taka, naomba ulichukua hili ili kuangalia namna ya kuanzisha Mamalaka za Maji taka ili kuhakikisha jamii zetu ziko salama" ameomba Nasri.

Akitoa shukrani za Wananchi wa Chumbi Diwani wa Kata hiyo, Ally Nguyu, ameishukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo Chumbi ambao utapunguza kero ya maji katika kata yake.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • BEREGE AKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA MOHORO.

    May 29, 2025
  • WAKUSANYA KODI RUFIJI WAPEWA MAFUNZO UKUSANYAJI WA KODI YA MAJENGO, PANGO LA ARDHI NA USHURU WA MABANGO.

    May 26, 2025
  • BEREGE AWATAKA WAFANYABIASHARA RUFIJI KUANZA KUJIANDAA NA KUZITUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI

    May 21, 2025
  • UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA CHIKICHI KUTOA AJIRA 5,000.

    May 16, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa