• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

RAIS SAMIA AMWAGA BIL. 50 BARABARA YA IKWIRIRI -MKONGO

Posted on: June 23rd, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha zaidi ya shilingi bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Ikwiriri-Mkongo iliyopo Wilayani Rufiji kwa kiwango cha lami yenye urefu wa km 27 pamoja na taa za barabarani, ambapo ujenzi utaanza hivi karibuni.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mkongo na Ikwiriri leo Juni 23, 2025.

"Rais Samia alishaidhinisha fedha kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Ikwiriri-Mkongo pamoja na taa za barabarani 180". Amefafanua Waziri Ulega.


Aidha, amesema dhamira ya Serikali ni kujenga barabara nyingine kutoka Chalinze- Mloka-Mkongo pamoja na ujenzi wa daraja la Kisasa,  litakalounganisha  Mkongo - Utete.


Vilevile  amesema Rais Samia ameridhia ujenzi wa Barabara ya njia nne ya kutoa Ikwiriri -mpaka Mkuranga.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa amemshukuru Mhe.Rais Samia  kwa  kutoa fedha ya ujenzi wa barabara hizo, ambazo zinakwenda kuunganisha Rufiji na kukuza uchumi wa Wananchi.

Amesema Barabara za Rufiji zilikuwa hazipitiki hasa wakati wa mafuriko.


Katika hatua nyingine wana umoja wa wanawake wa CCM Wilaya ya Rufiji wamefanya maandamano ya amani ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kumchagua Rais Samia.

Pia wamempatia Mhe waziri Mchengerwa cheti cha pongezi kwa kutambua mchango wake katika kuwapatia wananchi wa Rufiji maendeleo.

Katika ziara ya leo Mhe. Mchengerwa alikagua miradi mbalimbali ikiwemo kituo Cha Afya Cha Mkongo, Soko la Mhe. Mchengerwa na Shule ya Sekondari ya Mkongo na kutoa maelekezo ya kuboresha  huduma katika maeneo hayo.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA AMWAGA BIL. 50 BARABARA YA IKWIRIRI -MKONGO

    June 23, 2025
  • DC KOMBA AAGIZA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI ITOLEWE KWA KATA ZOTE RUFIJI.

    June 26, 2025
  • WATUMISHI WA UMMA RUFIJI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI, WASISITIZWA KUFANYAKAZI KWA BIDII, WAONYWA KUTOA HUDUMA KWA UPENDELEO MAOFISNI

    June 25, 2025
  • BEREGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA MKONGO, KIPUGIRA, NGORONGO

    June 11, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa