• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

KERO YA MAJI MIANGALAYA YABAKI HISTORIA

Posted on: March 30th, 2025

Wananchi wa Kitongoji Cha Miangalaya, Kijiji cha Nambunju Kata ya Mbwara Wilayani Rufiji Mkoani Pwani, wameendelea kutoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mbunge wa Jimbo la Rufiji na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohammed Mchengerwa, baada ya kujengewa mradi wa Maji na kutatua kero ya upatikanaji wa Maji safi na salama iliyokuwa ikiwakabili kwa muda mrefu, ikiwa ni ahadi ya Mbunge ya kumaliza tatizo hilo.

Haya yamedhihirishwa na Mwenyekiti wa Kitongoji Cha Miangalaya Bw. Bakari Muba maarufu (Bolwe) Wakati akishuhudia pamoja na Wanafunzi zoezi la kujengwa kwa Miundombinu ya maji katika shule ya Msingi Miangalaya iliyopo Kijiji Cha Nambunju Kata ya Mbwara, ambapo awali  wanafunzi na Wananchi hao walilazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 5 kutoka katika Kitongoji Cha Miangalaya kilichopo mpakani  mwa Wilaya ya Rufiji na Kilwa kufuata maji safi na salama katika eneo la Nambunju (Makao makuu ya Kijiji).

"... tunapokea mradi huu wa maji ambao RUWASA wametuunganishia ambao ni ahadi ya Mheshimiwa Mbunge toka mwaka 2017  kwamba tulimuomba mradi wa maji ufike  katika eneo la shule ya Msingi miangalaya, na Leo wanafunzi wanafurahia kwa maana walikuwa wakipata adha kubwa katika kipindi chote hiki Cha masomo walikuwa wanapata shida ya Maji. Kwahyo leo tumefanikiwa kupata mradi huu, kwa maana tunamshukuru Mheshimiwa Rais, Mbunge pamoja na Mheshimiwa Diwani lakini bila kusahau Wazee na Wananchi kwa Ujumla." Alieleza Bolwe.

Itakumbukwa kuwa shule ya Msingi Miangalaya ilijengwa kutoka kwenye kituo shikizi kilichokuwa na darasa Moja lililojengwa na Wananchi kwa kutumia udongo na miti ambapo mwaka 2018  kituo hicho kilipelekewa mifuko ya sementi na fedha ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa toka kwa Mbunge, na Mwaka 2021 walipokea fedha milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi, vyoo matundu manne iliyogharimu kiasi cha Shilingi milioni 4.4, matundu sita ya vyoo yaliyojengwa kwa Shilingi milioni 6.5 na kupelekea kituo hicho kuwa na usajili kamili wa Shule ya Msingi Miangalaya.

Hata hivyo Shule hiyo hivi Sasa imepokea Shilingi millioni 95 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Walimu ( 2 in 1).

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • SIRI YA RUFIJI KUMSHUKURU RAIS SAMIA NA MBUNGE MCHENGERWA

    May 09, 2025
  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa