• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

KAMATI YA BUNGE YATEMBELEA MAENEO YALIYOATHIRIKA NA MAFURIKO RUFIJI

Posted on: August 16th, 2024

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira wametembelaea maeneo yaliyoathirika na mafuriko katika Kata ya Mohoro Wilayani Rufiji, ambapo walitembelea Shule ya Msingi Mohoro, Kituo cha Afya Mohoro pamoja na kuangalia eneo ambapo limetengwa na serikali kwa ajili ya kugawa viwanja kwa Wananchi wa Kata ya Mohoro ambao walikuwa wanaishi kwenye maeneo ya njia ya maji (mabondeni).

Kamati hiyo ilifanya ziara Ijumaa Agosti 16, 2024 pamoja na kuzungumza na Wananchi katika Kijiji cha Shela Kata ya Mohoro baada ya Kamati hiyo kuangalia maeneo yaliyoathirika na mafuriko na kutoa pole kwa Wananchi, huku Mwenyekiti  wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  Maji na Mazingira  Jackson Kiswaga aliwataka Wananchi kuchangamkia fursa ya Viwanja vilivyoanza kugaiwa na Seikali na kutoka maeneo ya mabondeni ili kuepuka athari za mafuriko.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Mhe. Abdul Chobo aliomba Serikali iwasaidie kuwaongezea viwanja ili Wananchi waliokuwa wanaishi kwenye maeneo ya mabondeni waweze kuhama katika maeneo hayo na kuepuka athari ya mafuriko.

“viwanja  vimepata Vijiji viwili Kijiji cha Shela na Kijiji cha King’ongo lakini Mohoro Mashariki na Mohoro Magharibi hata Mwananchi mmoja hajapata Kiwanja, tunakuomba Mwenyekiti wa Kamati (Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira) uondoke na hili ili Serikali itusaidie kupatata Kiwanja”

“tumesikia Wananchi wakisaidiwa kupelekewa misaada ya kujengewa majumba, tumesikia Wananchi wakijengewa majumba ya kukopeshwa ili walipe kidogo kidogo, tunaomba  na sisi tusaidiwe kwasababu hali zetu ni ngumu” aliongeza Mhe. Chobo huku kushangiliwa na mamia ya Wananchi.

 Akilizungumzia jambo hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  Maji na Mazingira Mhe.  Jackson Kiswaga alisema swala hilo wamelichukua  na wanakwenda kulifanyia kazi huku akiwataka Wananchi kuchangamkia fursa ya Viwanja vilivyoanza kugaiwa na Seikali na kutoka maeneo ya mabondeni ili kuepuka athari za mafuriko.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Khamis  Hamza Khamis amepiga marufuku  tabia ya ukati wa miti ovyo pamoja kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo uvuvi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge pamoja na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Rufiji ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanal Joseph Kolombo walikuwa wenyeji wa kuitembeza Kamati hiyo katika maeneoyaliyoathirika na mafuriko.

Mohoro ni moja ya kati ya Kata 13 za Rufiji zilizoathirika na mafuriko yaliyotokana  na mvua kubwa zilizonyesha mapema mwaka huu ambapo katika kukabiliana na changamoto hizo  Mpaka sasa Serikali imeshatenga viwanja takribani 600 bure kwa ajli ya Wananchi wa Kata ya Mohoro ikiwa ni pamoja na eneo la kujengwa Shule mpya ya msingi pamoja na Kituo cha Aya.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa