• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

GOWELE: TUTENGE MAENEO KWA AJILI YA UWEKEZAJI, KILIMO, MAKAZI

Posted on: July 2nd, 2024


Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele, amezitaka halmashauri za vijiji na Vitongoji kutenga maeneo ya uwekezaji, kilimo pamoja na makazi ili kuepuka migogoro baina ya Kijiji na wawekezaji wanaowekeza katika maeneo mbalimbali Wilayani Rufiji.

Gowele amesema kutenga maeneo hayo kutasaidia Wananchi kujua maeneo rasmi ya kilimo hali itakayosaidia kutovamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na kufanya kufanya shughuli za kilimo.

‘’hatuwezi kukataa uwekezaji, tutenge eneo kwa ajili ya uwekezaji, kwa ambao watafanya uwekezaji, tuwe na eneo la kilimo na tuwe na eneo la makazi’’ alisema DC Gowele.

Gowele aliyazungumza hayo katika kikao na Wananchi wa Kitongoji cha Siasa Nyamakulukulu iliyopo Kata ya Utete Wilayani Rufiji leo Jumanne Julai 2, 2024 baada ya kupokea malalamiko ya Wananchi wa Kitongoji hicho kuwa kuna Muwekezaji katika eneo hilo ameweka bikoni (alama za mipaka) katika makazi ya Wananchi na kwenye mashamba yao.

Katika kutafuta namna bora ya kutatua mgogoro huo DC Gowele ameunda kamati maalumu ya ufuatiliaji na upimaji wa eneo alilopewa mwekezaji awali, ili kubaini ukubwa wa ardhi iliyoombwa Wakati huo, ikilinganishwa na idadi ya wakazi wa Kijiji hicho Kwa Sasa kisha kutoa mrejesho Kwa wanakijiji ili waweze kutoa eneo la uwekezaji bila kuathiri makazi na maeneo ya kilimo kwa wanakijiji hao.

"na muwekezaji awe tayari kupunguza eneo baada ya kulihakiki, eneo lichorwe upya, hizo bikoni zilizowekwa huko mimi sizitambui, zitoke muanze upya kwa kushirikana na Kamati niliyounda hapa’’ alisema Meja.

Pia Gowele amewataka Wananchi wanaofanya shughuliza kilimo katika maeneo ya uwekezaji wa Kijiji au Kitongoji waombe kwa kufuata taratibu za Kijiji husika.

"wajibu wangu ni kusimamia, na kama unazo heka 200 utatuambia umepata wapi! Kama ulipewa kwa utaratibu wa Kijiji, Kijiji kina uwezo wa kutoa mwisho heka 50’’ alisema DC.

Mbali na hayo pia, Mkuu huyo amepiga marufuku uuzaji wa pombe za kienyeji majumbani kwasababu itasababisha mmonyoko wa maadili kwa Watoto, huku akiwataka kuwa na eneo maalumu litakalotambulika kwa ajili ya biashara hiyo.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • BEREGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA MKONGO, KIPUGIRA, NGORONGO

    June 11, 2025
  • BEREGE AKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA MOHORO.

    May 29, 2025
  • WAKUSANYA KODI RUFIJI WAPEWA MAFUNZO UKUSANYAJI WA KODI YA MAJENGO, PANGO LA ARDHI NA USHURU WA MABANGO.

    May 26, 2025
  • BEREGE AWATAKA WAFANYABIASHARA RUFIJI KUANZA KUJIANDAA NA KUZITUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI

    May 21, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa