• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

DC Gowele Apokea Saruji 100 za Ukarabati wa Madarasa, Nyumba ya Mwalimu

Posted on: December 9th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele, amepokea na kukabidhi mifuko 100 ya saruji kutoka Chama cha Ushirika cha Mkoa wa Pwani CORECU, kwa ajili ya ukarabati wa madarasa mawili na nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Sekondari Muhoro, ikiwa ni arambee aliyoianzisha Novemba 5 mwaka huu.

Wadau wengine waliounga mkono ni banki ya CRDB mifuko 25, NMB mifuko 15 pamoja na Wananchi walioahidi kuchangia jambo hilo. CORECU, CRDB na NMB ni moja ya wadau walioahidi kuchangia mifuko ya saruji.

“Nawashukuru wadau wote ambao mmejitoa kuchangia jambo hili, leo nimepokea na nimekabidhi kwenu mifuko hii (saruji) ili ikiwezekana vianze kazi. Pia niwashukuru Wazazi ambao mlikubaliana wenyewe kwamba kila Mtoto mtachanga shilingi 1000, mmeonesha dhamira ya kuchangia miundombinu ya shule hii” amesema DC Gowele.

Makabidhiano hayo yamefanyika Disemba 8, 2023 katika shule ya Sekondari Muhoro huku akiwataka Wananchi na kamati iliyokabidhiwa mifuko hiyo kuhakikisha inatumika kama ilivyokusudiwa.

“ikitokea mmoja wetu akahujumu maana yake tutakuwa tunawadhulumu hawa Watoto, matarajio yao ni makubwa kuhakikisha miundombinu yao inakamilika na Walimu wao wanakaa katika mazingira salama. Mimi nitasimamia hii arambee mpaka mwisho” amekemea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha CORECU Mussa Mng’aresa amesema kama chama wameguswa baada ya kupata taarifa, ndio maana wakaamua kutoa mchango.

“Mheshimiwa nilikuahidi nitaleta mifuko 100, hii ni mifuko ya Chama Kikuu CURECU”amesema Mng’aresa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Muhoro, Abdul Chobo amewashukuru wote waliotoa michangao yao, huku akitoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuchangia katika jambo hilo.

Akizungumza Mkuu wa Shule ya Sekondari Muhoro, amesema Disemba 5 2023 waliamua kuanzisha arambee baada ya kuona uchakavu wa madarasa mawili na nyumba 1 ya mwalimu.

Vilevile DC Gowele ameendelea kuwataka Wananchi kutunza miradi inayotekelezwa na serikali katika maeneo yao.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa