• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

BONANZA LAWASHA MOTO UTETE

Posted on: August 29th, 2020

ilikuwa patashika nguo kuchanika. aliyevaa pensi , sketi, suruali ya michezo, kandambili, viatu vya kukimbilia, kanga na nguo za sikukuu, Vijana kwa wazee na watoto kwa wakubwa. Kuanzia bomani kwenda mitaa yote ya Utete mpaka kiwanja cha mpira wa miguu cha Azimio, Mirindimo ya Nyimbo  na Vifijo kona zote za Utete zilisikika zikisema “ RUFIJI TWENDE PAMOJA…….” . Ni Bonanza la michezo lilofanyika tar. 29/08/2020 lenye kauli mbiu RUFIJI TWENDE PAMOJA ambalo lilianza kwa kukimbia mchakmchaka saa 12 asubuhi na baadaye michezo mbalimbali kuchezwa uwanjani ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, kuvuta kamba, kukimbia ukiwa ndani ya gunia, kuimba, kucheza muziki wa singeli na Bongo fleva, kukimbiza kuku, wazee kutunga uzi kwenye sindano, na mchezo wa kufunga kamba mguuni na kukimbia wawiliwawili. Wananchi walijitokeza kwa wingi katika bonanza hilo na kushiriki kikamilifu huku baadhi yao wakiibuka na Ushindi,  wakijizolea mazawadi ya pesa tasilimu papohapo na zawadi nyingine kemukemu zikiwemo masanduku ya soda na kuku.

Kwa upande wa Mpira wa miguu, mtanange ulianza kati ya Walimu na Watumishi wa Halmashauri ambapo walimu walishinda kwa matuta 04 kwa 03. Mechi nyingine ilikuwa ni kati ya bodaboda na chama cha mapinduzi ambapo chama cha mapinduzi iliibuka na ushindi na baadaye walimu kucheza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Utete  na Wanafunzi hao kuibuka na Ushindi.

Kwa upande wa kukimbiza Kuku Mh. Hawa Mtopa Diwani Mstaafu aliibuka na ushindi kwa uhodari wake wa kumrukia kuku na kumnyakua kama goli kipa anyakuavyo shuti kali la mpira lililoelekezwa golini kwake. kwa wanaume mshindi alikuwa mzee Hamisi Athumani ambaye naye alipotea ghafla mithiri ya kivuli uwanjani hapo, kwenda kumtengeneza kuku huyo kwa kitoweo cha siku. kila mmoja alifurahi sana. Katika mchezo wa kuvuta kamaba watumishi wa serikali kuu walionekana kuwa ndio walioshiba kuwazidi nguvu walimu. kwa upande wa wazee kutunga uzi kwenye sindano tano Mzee salum Athumani ilijibebea ushindi dhidi za wazee wenzake kwa kutunga sindano tatu.

Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye Mgeni rasmi kwenye bonanza hilo, amewashukuru na kuwapongeza wananchi kwa ushiriki Mkubwa katika tukio hilo la kihistoria na kuwaambia wanarufiji kuwa mambo mengi yamewezekana na watu kushinda kwasababu ya kuelewana na kukubalina namna ya kwenda pamoja na ndio maana wengi waliofanya hivyo wameshinda. “ wanarufiji tukielewana na kukubaliana tutakwenda pamoja na tutapata mafanikio makubwa. Huu ni mwanzo tu, tunaweza kupanga kila mwisho wa wiki kufanya mazoezi ya pamoja kama tulivyofanya leo. zamu ijayo ni zamu ya Ikwiriri.” Alisema.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • BEREGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA MKONGO, KIPUGIRA, NGORONGO

    June 11, 2025
  • BEREGE AKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA MOHORO.

    May 29, 2025
  • WAKUSANYA KODI RUFIJI WAPEWA MAFUNZO UKUSANYAJI WA KODI YA MAJENGO, PANGO LA ARDHI NA USHURU WA MABANGO.

    May 26, 2025
  • BEREGE AWATAKA WAFANYABIASHARA RUFIJI KUANZA KUJIANDAA NA KUZITUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI

    May 21, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa