• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

Bodi ya Afya Yazinduliwa Rufiji.

Posted on: November 3rd, 2023


Katibu Tawala (DAS) Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani Ayubu Sebabili, ameitaka Bodi ya Afya kuwa chachu ya Maboresho ya Miundombinu na huduma za Afya kwa Wananchi kwani wao ndio kiunganishi cha Wananchi na Serikali katika sekta ya Afya.

DAS Sebabili ameyasema hayo leo Novemba 2, 2023 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi ya Afya Wilaya ya Rufiji iliyofanyika katika ukumbi mdogo wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.

“ Mtoe mawazo yenu katika mapitio ya bajeti za Afya kutokana na mahitaji halisi mnayoyasikia na kuyaona kwa Wananchi. Mkashauri namna bora ya kuboresha mapato yatakayowezesha kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa jamii.” Alisisitiza Katibu tawala.

Sanjari na hayo ameitaka bodi hiyo kuwa sehemu ya mshikamano kwa Watumishi na kuacha kuwa chanzo cha maneno ya uchochezi yatakayoondoa ari ya kazi na ufanisi kwa watumishi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Abdul Chobo ameipongeza bodi hiyo kwa kuaminiwa na kuchaguliwa huku akiweka bayana kuwa Halmashauri ipo tayari Kushiriki na kusimamia yale ambayo bodi hiyo itapendekeza na kuyaleta Halmashauri kwa manufaa ya Jamii .

“ tunategemea uwepo wenu mtatusaidia kuwajengea wananchi uelewa juu ya jitihada na huduma zinazotolewa na Serikali kwa Wananchi wake kwani Afya ndio msingi wa maendeleo ya jamii yoyote ile.” Alisisitiza Mwenyekiti.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Sebastian Gaganija amemtaka Mganga Mkuu Wilaya ya Rufiji kuhakikisha bodi hiyo inajengewa uwezo ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na ubunifu Mkubwa.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA CHIKICHI KUTOA AJIRA 5,000.

    May 16, 2025
  • SIRI YA RUFIJI KUMSHUKURU RAIS SAMIA NA MBUNGE MCHENGERWA

    May 09, 2025
  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa