• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

60 teachers trained on students performance improvement

Posted on: June 3rd, 2018

Jumla ya walimu 60 wa masomo ya Fizikia, Kemia, Elimu ya Viumbe, Hisabati na Kiingereza wapatiwa mafunzo ya namna ya kufundisha masomo hayo kwa ufasaha. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi Ikwiriri kwa muda wa siku 2 mfululizo kuanzia jana.

Akiongea wakati wa ufunguzi; Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Bw: Mussa A. Lambwe aliwaasa washiriki wote kuwa makini na kufuatilia mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wawezeshaji wa kitaifa waliofika kutoa mafunzo hayo. Alisistiza kuwa semina ina lango la kuwajengea uwezo walimu wa masomo ya sayansi na lugha ya kiingereza. Kila mshiriki alikumbushwa kuwa ana jukumu la kwenda kuwafundisha walimu wengine katika kituo chake cha kazi yale yaliyofundishwa katika semina hiyo. 

Washiriki wa mafunzo hayo walikumbushwa na kufundishwa mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na jinsi ya kutumia njia shirikishi, kulitawala darasa, kuandaa mpango kazi wa somo, kuepuka kutumia adhabu ya kuchapa fimbo kwa lengo la kujenga nidhamu ya wanafunzi, kuwatambua wanafunzi kwa uwezo wao kimasomo, kutumia malighafi za kienyeji zinazoweza kupatikana bure au kwa bei nafuu katika kuandaa masomo kwa njia ya vitendo.

Hata hivyo walimu walitoa baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo katika kutekeleza majukumu ya kila siku. Muda ni mfupi pale mwalimu anapoamua kutumia njia shirikishi katika kufundisha. Njia shirikishi inachukua muda zaidi ukilinganisha na njia ya kawaida ya kufundisha ambapo mwalimu huwasilisha kile alichokiandaa kwa mujibu wa ratiba na mpango kazi wa somo lake kwa wanafunzi.

Kutokutumia adhabu ya kuchapa fimbo kurekebisha nidhamu ya wanafunzi nayo inaonekana ni changamoto kwani walimu wengi huona kama ni njia rahisi ya kumrudi mwanafunzi na huchukua muda mfupi ukilinganisha na njia nyingine.

Vilevile kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari ukilinganisha na hapo awali. Darasa moja linakuwa na idadi kubwa ya wanafunzi ukilinganisha na uhalisia wake hivyo kupelekea mwalimu kumfikia kila mwanafunzi kipindi cha masomo ya darasani.

Mkufunzi wa mafunzo hayo Bw: Ramadhani Matimbwa aliwaasa walimu kutumia njia mbadala kujenga nidhamu ya wanafunzi badala ya fimbo. Alisema kuwa fimbo ina madhara makubwa sana kwa mwanafunzi ukilinganisha na faida zake; mojawapo ikiwa ni pamoja na kutengeneza chuki baina ya mwanafunzi na mwalimu, nidhamu ya woga,  maumivu makali ya mwili na kusababisha baadhi ya wanafunzi kukatisha masomo. 

Matokeo ya mafunzo hayo ni pamoja na kujenga nidhamu bora ya wanafunzi bila kutumia fimbo, kutumia njia shirikishi katika kufundisha hivy kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya ngazi tofauti ikiwemo ya kitaifa. 

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa