• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

WAZAZI WAKUBALIANA WANAFUNZI WALE SHULENI

Posted on: February 29th, 2024

Wazazi wa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kazamoyo, Kata ya Ikwiriri Tarafa ya Ikwiriri Wilayani Rufiji Mkoani Pwani, wamekubaliana kwa pamoja kutoa michango ya shilingi 500 kwa siku ili wanafunzi wapate Chakula cha pamoja wakiwa shuleni hali itakayosaidia kuongeza hamasa ya kusoma kwa bidii.

Wazazi  walikubaliana hayo kwenye Mkutano wa elimu kati ya Wazazi na Walimu uliolenga kujadili namna kuinua ufaulu wa kitaaluma kwa Wanafunzi shuleni hapo jana Februari 29, 2024 uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Kazamoyo.

“tumekubaliana kila mzazi atatoa 500 kwa siku shilingi 2000 kwa Wiki, kwasababu inatakiwa mtoto ale shuleni ili apate elimu Shuleni” alisema Sharifa Sobo Mzazi wa Mwanafunzi katika shule hiyo.

Mbali na hayo  Wazazi hao wamekubaliana Kushirikiana na Walimu pamoja na Ofisi ya Mtendaji Kata kutokomeza tabia ya utoro na kusimamia nidhamu kwa Wanafunzi ikiwa ni pamoja na kukemea baadhi ya tabia za wazazi lushiriki kuficha watu wanaowapatia ujauzito watoto wao.


Akieleza baadhi ya changamoto  Mkuu wa Shule ya sekondari Kazamoyo Ramadhani Kazee  alisema kuna baadhi ya Wanafunzi hukaa vichakani muda wa masomo wakivuta bangi na kutoa lugha za matusi kwa walimu wanapowafuatilia.

 “Wazazi wameonyesha kwamba watakuwa bega kwa bega na shule ili kuhakikisha nidhamu ya hapa shuleni inakuwa bora kwa vijana wao, na tayari kwa ajili ya kupata elimu iliyokuwa bora” aliongeza Kazee.

kuhusu swala la lishe kazee alisema “sisi kama shule tayari tulishajipanga, tayari tulikuwa tumeshaanza hamasa kwa Wazazi, kabla ya kikao cha leo wapo baadhi ya Wanafunzi wapatao 32 walikuwa wakila pamoja na wenzao wa hosteli na bweni”

Kwaupande wake, Afisa Mtendaji Kata ya Ikwiriri Exavery Likwembe,  alisema kuhusu Chakula shuleni ni sera ya serikali hivyo amewaomba Wazazi Kushirikiana ili kufanikisha jambo hilo kama Walivyokubaliana huku akisisitiza kuwa atasimamia yale yaliyokubaliwa.

Balozi wa Elimu Wilayani Rufiji, Bashir Kibopo aliwasisitiza Wazazi kuhakikisha wanashirkiana na Walimu ili watoto wapate elimu ambayo itawasaidia katika maisha yao baadae.

“hakuna ulithi muhimu kama ulithi wa elimu hata wewe ukifa elimu atabaki nayo yeye, itamuongoza yeye na aliyesoma kasoma tu, kwahiyo me niwaombe kina mama (wazazi) tuhakikishe mtoto anapata elimu” alisisitiza Kibopo.

Ally Ndungutu Diwani wa Kata ya Ikwiriri aliwapongeza wazazi kwa kuamua Kushirikiana na Walimu kuhakikisha watoto wanapata Chakula shuleni, kutokomeza utoro na kubainisha kuwa kufanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ambayo imetoa fedha za miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule mpya katika kata hiyo.


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa