• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

WANASHERIA WATOA ELIMU RUFIJI

Posted on: February 1st, 2024

Wananchi wa Kata ya Chumbi Wilayani Rufiji Mkoani Pwani wamepata semina ya namna ya umiliki wa ardhi, vyombo vya usimamizi wa ardhi, pamoja na vyombo vya utatuzi wa migogoro ya ardhi, hali itakayopelekea kupunguza migogoro katika maeneo yao.

Semina hiyo imefanyika leo Februari 1, 2024 katika kijiji cha Chumbi C, kata ya Chumbi kwenye ukumbi wa Kijiji hicho, yenye lengo la kuangalia haki ya Mwanamke katika umiliki wa ardhi, ikiwa ni kampeni ya Linda Adrhi ya Mwanamke ‘Stand For Her Land’, iliyoandaliwa na mashirika mbalimbali ikiwemo Jukwaa la Ardhi Tanzania, Shirika la kutetea haki za binadamu LHRC, Shirika linalofanya kazi na serikali na mashirika ya ndani kupata haki za sheria za ardhi kwa familia masikini LANDESA, Shirika la sheria kiganjani na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania.

Wananchi wa Chumbi walitumia fursa hiyo kueleza matatizo yao ya migogoro ya ardhi na kuomba msaada wa kisheria na kusaidiwa njia zipi wapite ili kupata haki zao, ambapo Pili Mnema Mkazi wa Kijiji cha Chumbi C alidai Baraza la ardhi la Kata lilitoa maamuzi ya kumshindisha kesi Mwananchi huyo alipokuwa kwenye kesi ya Mgogoro wa ardhi.

Akitoa ufafanuzi juu ya maamuzi yaliyofanywa na Bazaraza hilo, Mwanasheria Nuru Pipino amesema hukumu hiyo ni batili kwasababu Baraza la Kata halina uwezo wa kutoa maamuzi ila lina mamlaka ya kufanya usuluishi na kutoa hati ya mgogoro kama umeshindikana kusuluishwa, ili kesi iendelee ngazi nyingine.

 “na baada ya hapo kupitia ile hati utaenda baraza la nyumba ya ardhi ya Wilaya kufungua kesi upya” amefafanua.

Baada ya mafunzo hayo katika mahojiano binafsi na baadhi Wananchi wamewapongeza walioandaa semina hiyo ambayo imetoa elimu kwa Wananchi juu ya masuala ya kisheria.

Kwa upande wake Wakili kutoka Shirika na utetezi wa haki za binadamu LHRC, Aneth Kaganda amewasisitiza Wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kufanya maamuzi ya maendeleo katika maeneo wanayoishi.

Kampeni hiyoimefanyika katika kata 3, Utete, Chemchem na Chumbi.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA AMWAGA BIL. 50 BARABARA YA IKWIRIRI -MKONGO

    June 23, 2025
  • DC KOMBA AAGIZA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI ITOLEWE KWA KATA ZOTE RUFIJI.

    June 26, 2025
  • WATUMISHI WA UMMA RUFIJI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI, WASISITIZWA KUFANYAKAZI KWA BIDII, WAONYWA KUTOA HUDUMA KWA UPENDELEO MAOFISNI

    June 25, 2025
  • BEREGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA MKONGO, KIPUGIRA, NGORONGO

    June 11, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa