• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MATUMBAWE

Posted on: February 23rd, 2024

Serikali Wilayani Rufiji Mkoani Pwani imewataka Wananchi hususani wanaojishughulisha na Uvuvi pamoja na mazao ya bahari kuacha kuharibu miamba ya makuzi ya vizalia vya viumbe hai Wanaoishi baharini (Matumbawe) ili kutunza uhai wa viumbe hivyo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele wakati akifungua mafunzo ya namna ya uhifadhi wa miamba ya makuzi ya vizalia vya viumbe hai wanaoishi baharini yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri Februari 23, 2024.

“niombe Wadau mlioshiriki hapa leo ndo maana tumejumuisha na Wavuvi, tusipotunza maana yake kesho hatutauza na hatutazalisha kwa sababu sisi tunajua nani anavua kwa kutumia uvuvi haramu mfano wa baruti, kwahiyo tukawe wakali vinginevyo tutapoteza hizi spicies (viumbe hai) katika maeneo yetu” Alisisitiza Meja Gowele

Akielezea faida ya miamba hiyo baharini Meneja wa Taasisi ya hifadhi ya bahari na maeneo tengefu Godfrey Ngupula amesema miamba hiyo ndio uhai wa viumbe hai wanaoishi baharini na kufafanua kuwa kutokuwepo kwa miamba hiyo itasababisha viumbe hao kukosa makazi maalumu ya kuzaliana na kutunza viumbe baharini ambapo moja ya jambo linaloweza kusababisha kuvunjika kwa miamba hiyo ni ukataji holela wa miti ya mikoko pembezoni mwa bahari.

 “matumbawe ni eneo dogo sana halizidi hata asilimia moja ya bahari yote, zaidi ya asilimia 80 ya Wavuvi wa kawaida wanategemea uhai wa matumbawe, kwahiyo Matumbawe ni miamba iliyopo baharini. Sasa kwenye ufukwe huku kua Matumbawe mengi sana ni zaidi ya upana wa km 1 mpaka 3 lakini pia ni marefu kuanzia Mtwara, Kilwa, Mafia, Kibiti, Rufiji (Mohoro), Tanga na Pemba. Sasa rasilimali hii lazima itunzwe” amesisitiza Ngupula.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji na Diwani wa kata ya Mohoro Abdul Chobo ameipongeza Taasisi hiyo kwa kutoa semina ya elimu juu ya umuhimu wa kutunza Matumbawe kwasababu Mohoro inapakana na Kibiti ambayo eneo nusu ya eneo lake lipo katika Matumbawe.

Akielezea namna alivyoyapokea mafunzo hayo, Yusuph Pakacha Mvuvi na Mkazi wa Hohoro amesema aatkuwa balozi mzuri wa kutoa elimu kwa Wavuvi wengine kuacha tabia ya ukataji wa miti ya mikoko na uvuvi haramu ili kutunza rasilimali hizo.

“nilichojifunza hapa ni kwamba Matumbawe hayafai kuyang’oa, kuyakata kwasababu ni mazalia ya samaki pamoja na kuacha ukataji wa miti ya mikoko” amesema.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa