• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

WAFUGAJI WARIDHISHWA NA MAAMUZI YA SERIKALI

Posted on: November 14th, 2020


Mkuu wa Wilaya Rufiji Luteni Kanali Patrick Sawala pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Ndg. Rashid Salum Salum amekutana na Wafugaji kwa mara ya pili katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo FDC- Ikwiriri Wilayani Rufiji, kwa lengo la kufanya tathmini ya Utekelezaji wa Makubaliano na maagizo yaliyotolewa  katika Mkutano maalum wa Wafugaji uliofanyika hapo awali  katika Ukumbi wa Serengeti Ikwiriri Wilayani humo. Pia Mkutano huo ulihudhiriwa na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wataalamu wa Mifugo na Kilimo ngazi ya Halmashauri, Kata pamoja Watendaji wa Kata zote Wilayani Rufiji.

Katika Mkutano huo Mhe. Sawala alifungua kwa kuwapa fursa Viongozi wa Chama cha Wafugaji Rufiji – Kibiti ambao aliwapa nasafasi ya kuwa mstari wa mbele katika ufuatiliaji wa Utekelezaji wa makubaliano kipindi chote cha utekelezaji.

AkIleza namna walivyoshiriki na kubaini Changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa maelekezo na makubaliano yaliyotolewa na kuafikiwa katika mkutano wa kwanza Katibu wa Chama cha Wafugaji Rufiji na Kibiti amesema Pamoja na kuwa Wafugaji wengi walitekeleza makubaliano lakini bado kulikuwa na Wafugaji ambao waliendelea kukaidi maelekezo zaidi walikuwa wakiendelea kupitisha mifugo yao kwenye mashamba ya Wakulima. “Siku moja Mkuu wa Wilaya alinipigia simu kwenda Nyamwage kujionea Wafugaji namna wananvyoendelea kukaidi makubaliano na maagizo. Tulipofika pale Nyamwage tukakuta kuna Mkulima analima na humohumo shambani kuna makundi makubwa matatu ya Ng’ombe yakiwa na Wachungaji. Kwakweli nilijisikia aibu sana. Wafugaji wale walichukuliwa hatua kali.” Alisema.

Baada ya ushuhuda huo na maelezo mengine toka kwa Katibu, Mkuu wa Wilaya aliwakaribisha Wafugaji ambao nao Walieleza Vikwazo vyao ikiwa ni baadhi ya Wakulima kuendelea kubaki katika maeneo ya  Wafugaji jambo ambalo limekemewa vikali na Mkuu wa Wilaya na kuagiza Viongozi kuhakikisha Wakulima Wote waliobaki maeneo ya Wafugaji wahame mara moja.

Naye katibu wa Chama cha Wafugaji aliwasilisha mapendekezo ya kutatua migogoro ya Wakulima na Wafugaji kuwa Serikali inatakiwa kuunda kamati maalum itakayokuwa inasimamia na kufatilia kwa Ukaribu swala la Mifugo katika Wilaya, kufanya Sensa maalum ya Mifugo yote na Wafugaji waliomo ndani ya Wilaya ili kuzuia uingiaji wa MIfugo kiholela, Kupitia Upya na kubainisha njia zote za Mifugo, pamoja na kuhamasisha Wafugaji kuingia katika Mfumo wa ufugaji wenye tija ambao ni ufugaji wa kisasa.

Aidha Bw. Ndaki ambaye ni Makano Mwenyekiti wa Wafugaji ameeleza kuwa wapo katika hatua za Mwisho kuanza mpango wa ufugaji wa kisasa na maziwa kwa Wilaya ya Rufiji.

Sambamba na hayo, Mwenyekiti wa Wafugaji amesisitiza juu ya Swala la Ufugaji wa Kisasa na Wenye tija ili Wafugaji waweze kunufaika na mifugo yao.

Mkurugenzi Mtendaji Ndg, Rashid SalumSalum amewakumbusha watendaji kuwajibika na kuwa chanzo cha masuluhisho kwani Wao ndio wanaomwakilisha yeye katika majukumu yao ya kila siku, hivyo wasiache kutatua changamoto wakisubiri kuzifikisha kwa Mkurugenzi wao wawe sehemu ya suluhsho badala ya kuwa sehemu ya kulalamika.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ametoa maelekezo kwa Wafugaji na Viongozi Waendeleee kusimamia vizuri swala la Mifugo hasa katika kuhakikisha inaenda katika maeneo yaliyopangwa, kukaa na Wakulima na Wafugaji ili kwa pamoja kuchagua na kuonyesha njia ya Mifugo kuelekea kwenye maji “ nataka majibu ya maelekezo haya niyapate siku ya alhamisi” Alisema. Pia amewaagiza maafisa mifugo kuwa karibu na Wafugaji ili kuweza kubaini na kutoa ushauri wa changamoto wanazoweza kukutananazo.” Ninataka kufikia siku ya jumatano nipate ratiba ya kila Afisa Mifugo inayoonesha tarehe, siku na mfugaji unayepanga kumtembelea katika Wiki, na Mwezi, sambamba na hayo ameagiza kuundwa kwa kamati za za wafugaji na wakulima kuanzia ngazi ya chini na kupelekewa kamati hizo

Vilevile ameagiza Wafugaji khudhuria mikutano ya Vijiji ilikuwa sehemu ya maamuzi ya makubaliano mbalimbali ndani ya Vijiji vyao.” Ninaagiza Viongozi mifugo isiingie mpaka mimi nijiridhishe.” Aliagiza.

Baada ya Mkutano huo Wafugaji wameishukuru sana Serikali kwa namna ambavyo inawajali kwa kuitisha mikutano ya mara kwa na kutoa nafasi ya kuelezea changamoto wananzokutananazo ambazo nyingiwameshuhudia zikipatiwa ufumbuzi.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa