• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

UTETE-KINGUPIRA YAANZA KUSAFISHWA KUJENGWA KWA TABAKA GUMU

Posted on: July 22nd, 2024

Barabara ya Utete-Kingupira  inajengwa kwa kiwango cha tabaka gumu kwa urefu wa kilomita 32 kwa thamani ya shilingi bil 4.7 ambayo itadumu kwa muda mrefu bila ya matengenezo ya mara kwa mara (kila mwaka), hali itakayosaidia kurahisisha mawasiliano ya barabara kwa Wananchi wa Kata ya Ngarambe kupata huduma kwa haraka katika makao makuu ya Wilaya yaliyopo Utete, ambapo Mkandarasi yupo eneo la kazi kwa kuanza kuisafisha

Akizungumza katika mahojiano binafsi ofisini kwake, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Rufiji Mhandisi Nilocaus Ludigery, amesema mwaka 2023/2024 walipokea fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara hiyo ambayo ilikuwa inasumbua kwa muda mrefu hasa kipindi cha mvua nyingi.

“tunafanya matengenezo ya barabara ya Utete-Kingupira yenye urefu wa kilomita 32 kwa thamani ya shilingi bilioni 4.7” alisema Ludigery.

Ludigery alisema Wilaya ya Rufiji ina mtandao wa barabara wa kilomita 523.51 ambapo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Wilaya ya Rufiji ilikuwa na bajeti ya bilioni 2.1

“lakini pia tulipata fedha za dharula kwa ajili ya kukabiliana na mafuriko yaliyotokea mwaka 2024 , tulikuwa na matengenezo ya kawaida na maeneo korofi yenye thamani ya shilingi bilioni 2.2, kwa bajeti hiyo tuliweza kutekeleza km 186.69, lakini pia imefanya kuongeza barabara za changarawe kwa km 10” aliongeza.

Kufuatia ujenzi wa barabara hiyo inayojengwa na kampuni ya NSRT, baadhi ya Wananchi wameeleza hisia zao ya jinsi kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo itakavyorahisisha mawasiliano huku wakiishukuru Serikali kwa jinsi ilivyoiona barabara hiyo na kuitengea fedha ya jinsi kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo itakavyorahisisha mawasiliano.

Fadhili mbale ambaye ni Mkazi wa Utete anayenufaika kwa kupata kazi katika usafishaji wa barabara hiyo amesema anaona namna Serikali inavyoboresha miundombinu ya barabara ambayo ilikuwa kero kwa Wananchi wa Ngarambe kuja Utete ambako kuna hospitali ya Wilaya.

“tunaona uboreshaji wa miundombinu, kwasababu miundombinu itakavyokuwa bora na services (huduma) zingine zitapatikana. Tunashukuru Mungu viajira vimetokea familia zinanufaika na tunaona uboreshaji wa miundombinu” alisema Mbale huku akiwa anafanya kazi ya kusafisha barabara.

Kwa upande wake Mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo Bw. Filbert amewaondoa wasiwasi Wananchi ambao watakuwa wanaitumia barabara hiyo kuwa itadumu kwa muda mrefu bila ya kufanyiwa marekebishi ya mara kwa mara, kwakuwa inatengenezwa kwa tabaka gumu.

“ni tabaka gumu ambalo linatengenezwa kwa changarawe ikichanganywa na kimiminika ambacho kinaimarisha udingo kubeba mzigo mzito (stablelized layer), ni tabaka gumu ambalo litaifanya hii barabara ipikike kwa muda Mrefu na nitabaka ambalo halimomonyoki kiurahisi kwahiyo barabara itadumu na itabeba mizigo mikubwa” alisema Mkandarasi.

Mwananchi Mwingine Lida Mayonga Mkazi wa Kata ya Ngarambe ambaye alizungumza baada ya gari ya abiria aliyopanda kunasa kwenye mchanga wakati wa usafishaji wa barabara hiyo ukiwa unaendelea, alisema kukamilika kwa barabara hiyo itasaidia hasa kupunguza gharama za usafiri kwa kwa sasa wanalazimika kulipa 10,000 kwa usafiri wa gari huku pikipiki ikiwa elfu 25,000 na kurahisisha mawasiliano ya kufika kwa wepesi katika hospitali ya Wilaya na kupata huduma.

“yaani changamoto gari utakuta imenasa njiani barabara mbovu, ukiangalia Utete kwenda Ngarambe ni kilometa chache sana lakini nauli tunalipishwa kubwa, tunalipa shilingi 10000 iwe Mtoto au Mkubwa, kwa Pikipiki elfu 25,000” alisema.

Amesema kabla ya kuanza kwa usafishaji wa barabara hiyo hali ilikuwa sio nzuri kwakuwa ilikuwa na mashimo makubwa ambayo huwa yanasababishwa na mvua zinazonyesha kila msimu.

Kutokana na hatua hiyo Mwananchi mwingine ameishukuru Serikali kuijenga barabara hiyo tabaka gumu ambalo litadumu kwa muda mrefu. “kwasababu inawekwa tabaka gumu sisi tunashukuru, kwasababu miundombinu ndo inatakiwa kwasababu ndo kila kitu, huduma kiwa nzuri hata sisis tunapata kwenda Wilayani kwa wakati” alisema Abed Alembene Mkazi wa Ngarambe.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA RUFIJI WAANZA MAFUNZO RASMI

    August 04, 2025
  • PINDA AZINDUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI MKOANI MOROGORO

    August 02, 2025
  • RAIS SAMIA AMWAGA BIL. 50 BARABARA YA IKWIRIRI -MKONGO

    June 23, 2025
  • DC KOMBA AAGIZA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI ITOLEWE KWA KATA ZOTE RUFIJI.

    June 26, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa