• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

TUMUWEKE MUNGU MBELE NA TUBADILI TABIA ILI KUONDOKANA NA MAAMBUKIZI MAPYA YA VIRUSI VYA UKIMWI: DC SAWALA

Posted on: December 1st, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Patrick Sawala ameyasema hayo  leo ambapo ameongoza maelfu ya Wananchi wa Wilaya ya Rufiji katika zoezi la kupima na kutoa damu kwa hiari ikiwa ni  sehemu ya  Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambayo kiwilaya yameadhimishwa katika kijiji cha Shela kata ya Mohoro Wilayani humo.

 Tukio hilo limehudhuriwa na Katibu tawala Wilaya Bi. Maria Katemana,Mwenyekiti Mteule wa Halmashauri Mhe. Juma Ligomba akiambatana na Makamo Mwenyekiti Mteule wa Halmashauri,  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Rashid Salum Salum, Kamati ya Usalama ya Wilaya, Watendaji mbalimbali ngazi ya Halmashauri , Kata na Vijiji pamoja na Maelfu ya Wananchi waliojitokeza katika tukio hilo.

Mhe. Sawala, amewataka Wananchi kuunga Mkono juhudi za Serikali katika kupambana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi huku akiwataka Vijana kubadili tabia na kuzingatia maelekezo ya Wataalamu wa Afya kuchukua  tahadhari za maambukizi ya Ugojnjwa huo. “ Ninawasihi kujiepusha na maambukizi mapya, kuchukua tahadhari na kuacha Ngono zembe”, kwa upande wa Wananfunzi Sawala amewataka wananfunzi kusubiri na kuzingatia jukumu lao ambalo ni kusoma. “ Wanafunzi msubiri! Someni msiharakie maisha jukumu lenu ni kusoma.” Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya amewasisitiza wazazi kuacha kulazimisha ndoa za Utotoni kwa Watoto wao. Pia amehimiza Wananchi kupima ili kujua Afya zao mapema na Waanze tiba kwa wakati pindi wanapogundua kuwa wameathirika.

Aidha Mhe. Sawala amewataka wale wote wanaoambukiza wenzao kwa makusudi waache mara moja kwani kufanya hivyo ni kutenda dhambi ya kubwa ya kuua. “ Ukimrubuni mtu na kufanyanaye ngono bila kinga hali ya kuwa unafahamu kuwa umeathirika, unatenda dhambi ya kuua”. Alisema

Sambamba na hilo, Mkuu wa Wilaya amevipongeza vikundi vya sanaa vilivyotoa Burudani zilizobeba Ujumbe mzito wa Kuelimisha jamii dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Pia ameagiza kutunza na kuendeleza sanaa ya ushairi kwa kuhakikisha kila shule inakuwa na Wanafunzi wanaoweza kutunga kutunga mashairi. “ Navipongeza Vikundi vyote vya Sanaa vilivyotoa burudani hususani mzee Omary Mbonde pamoja na mzee Mwelekwa ninaagiza Wazee hawa wawe wanaalikwa katika Shughuli zote za Wilaya “.Alisema.

Akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi, Afisa Maendeleo ya Jamii ameeleza mafanikio yaliopatikana kaika Wilaya ya Rufiji,” Mafanikio yaliyopatikana katika kupambana na janga la UKIMWI  ni kuviwezesha  vituo 28 kutoa huduma za VVU/UKIMWI ambavyo vituo 11 vinatoa dawa za kupunguza makali ya VVU (CTC) na 17 vinatoa huduma za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). 

Ili kuhakikisha huduma zinawafikia walengwa kirahisi kuna watoa huduma za majumbani (Home Based Care Providers) 41 katika Kata 13 za Wilaya ya Rufiji 

Vilevile tunawaelimishaji rika 23 waliopatiwa mafunzo kupitia shirika la THPS, mwaka 2018. Kati ya hao 15 wanaendelea kutoa huduma katika vituo vyetu 11 vinavyotoa huduma kwa wateja wanaoishi na VVU/UKIMWI. Tumefanikiwa kuwapatia bima ya Afya iliyoboreshwa zaidi ya Vijana  172 wanaoishi na maambukizi ya VVU katika Halmashaurin ya Wilaya ya Rufiji ikiwa ni mchango kutoka katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na shirika la THPS ambao wamekuwa wadau wetu katika mapambano dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI kwa muda mrefu sasa. Alisema

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya Bi. Maria katemana amewapongeza Wananchi kwa kujitokeza kwa Wingi katika maadhimisho hayo na kuwasihi kuzingatia jumbe zinazotolewa katika maadhimisho hayo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndg, Rajshid Salum Salum amewataka Wananchi kuacha tabia za Unyanyapaa na kusisitiza kuwa Ukimwi upo hivyo tahadhari na kupima ni mambo muhimu ya kuzingatia” Ukimwi upo, tupime afya zetu, tusiwanyanyapae wenzetu tushikamane ili tuwe kitu kimoja.” Alisema.

Zaidi ya Wananchi 115 walijitokeza kupima na kuchangia damu ambapo kwa takwimu za madaktari na wataalmu wa afya waliokuwa wakiendesha zoezi hilo wamesema hakuna aliyekutwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Wilaya ya Rufiji mpaka hivi sasa takwimu zinaonesha kuwamaambukizi mapya  ni asilimia 1.6 tu.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa