• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

TUMIENI MBINU ZA KIBIASHARA KUHAKIKISHA MIRADI YA SERIKALI INAPATA VIFAA VYA UJENZI. TUIWEKE RUFIJI YETU MBELE: Patrick Sawala, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji

Posted on: January 7th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Patrick Sawala amewataka Wafanyabiashara wa Vifaa vya ujenzi Rufiji kutoa kipaumbele cha usambazaji wa vifaa katika miradi ya Serikali hasa katika Shule za Sekondari ambazo zimo katika kampeni ya ujenzi wa madarsa 13  yanayotarajiwa kupokea Wanafunzi awamu ya pili 650 wa Kidato cha kwanza 2021 kufikia tarehe 28/2/2021.Sawala ameyasema hayo alipokuwa katika kikao maalum cha Wafanyabiashara pamoja na Watendaji kata, lengo kuu likiwa ni kujadili hali ya utekelezaji wa miradi hiyo na changamoto zinazoweza kusababisha miradi hiyo kuchelewa kumalizika. “ tumieni mbinu za kibiashara kuhakikisha miradi ya serikali inapata vifaa vya ujenzi. Tuiweke Rufiji yetu mbele.”Alisema.Sambamba na hilo, amewataka watendaji na wasimamizi zikiwemo kamati za ujenzi wa madarsa hayo, kuagiza vifaa mapema ili vipatikane kwa wakati. “ Wasimamizi agizeni vifaa mapema ilivipatikane kwa wakati.” Alisema.AIdha amesisitiza kuwa shughuli zote za ujenzi ziende pamoja na utengenezaji wa viti na meza pamoja na madirisha ili kuendana na wakati na kuwa ifikapo tarehe 10/02/2021 zoezi hili liwe limekamilika. “ shughuli zote za ujenzi ziende pamoja. Ikifika tarehe 30 januari madawati na madirisha yawe tayari.” Alisema. Pia amewataka Watendaji kutoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi ikiwa picha ya jengo au majengo kila inapokamilika hatua moja kwenda nyingine na kutoa taarifa kwa haraka pale inapotokea changamoto. Amewataka watendaji wa halmashauri wanaohusika na miradi hiyo kutoweka urasimu wa aina yoyote ilikuhakikisha miradi inatekelezeka kwa wakati uliopangwa. “ Sitarajii kumuona mhandisi ofisini amekaa tu, sitarajii kusikia urasimu wa aina yoyote. naomba tuchukulie ujenzi huu kama operesheni. Hatutakiwi kushindwa na hatuna sababu ya kushindwa.” Alisema.Awali, Wafanyabiashara hao pamoja na Watendaji waliitaja changamoto ya ukosekanaji wa sementi kwa wakati na kwa idadi ndogo kulinganisha na mahitaji kuwa ni changamoto kubwa inayoweza kurudisha nyuma juhudi za ukamilishaji wa miradi hiyo kwa wakati uliopangwa. Pia, Wafanyabiashara wametoa angalizo la upandaji wa bei kwa bidhaa nyingine kama vile nondo unaoweza kupelekea shida kwa wanunuzi hasa katika kipindi hiki cha ujenzi.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA AMWAGA BIL. 50 BARABARA YA IKWIRIRI -MKONGO

    June 23, 2025
  • DC KOMBA AAGIZA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI ITOLEWE KWA KATA ZOTE RUFIJI.

    June 26, 2025
  • WATUMISHI WA UMMA RUFIJI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI, WASISITIZWA KUFANYAKAZI KWA BIDII, WAONYWA KUTOA HUDUMA KWA UPENDELEO MAOFISNI

    June 25, 2025
  • BEREGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA MKONGO, KIPUGIRA, NGORONGO

    June 11, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa