• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

TUHAKIKISHE TUNATEKELEZA KWA UFANISI NA KWA WAKATI AGIZO LA UTAMBUZI WA MAJENGO, VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI PAMOJA NA MABANGO ILI TUWEZE KUKUSANYA KODI KAMA ILIVYOAGIZWA:

Posted on: February 18th, 2021

Katibu Tawala Wilaya ya Rufiji Bi. Maria Katemana amewataka wahusika wote wanaohusika katika zoezi la ukusanyaji wa kodi za majengo, mabango pamoja na vitambulisho vya ujasiriamali kufanya kazi kwa ufanisi na kwa wakati ili kuweza kutekeleza agizo hilo kwa wakati.

Ameyasema hayo wakati akitoa maelekezo ya Serikali katika baraza la madiwani halmashauri ya wilaya rufiji lililokaa tarehe 18/2/2021 kujadili taarifa za robo ya pili 2020/2021 ambapo amesisitiza umakini katika utekelezaji wa sehemu ya kwanza ambayo ni utambuzi wa majengo, vitambulisho vya ujasiriamali pamoja na mabango ili kupata taarifa za uhakika zitakazorahisisha zoezi la ukusanyaji pindi litakapoanza.

 Aidha ametoa msisitizo kwa upande wa vitambulisho vya wajasiriamali kubaini wale waliokuwa wamepewa mwanzo na kuangalia maeneo ambayo yalikuwa changamoto wakati wa zoezi hilo ili kuboresha wakati wa kuanza zoezi kwa mara nyingine. “ Tubaini wale  waliopewa mwanzo na tuangalie wapi tulikwama mpaka kufikia kutokamilisha zoezi lile kwa ukamilifu.”Alisema

Sambamba na hilo ametoa msisitizo juu ya kukamilisha kwa wakati ujenzi wa vyumba 13 vya madarasa na kukabidhi ifikapo tarehe 22/02/2021. “ Tuhakikishe tunakamilisha zoezi la ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wakati kwani mpaka jana nimepokea taaifa kuwa madarsa yaliyokamilika ni mawili ya shule ya sekondari kazamoyo na mengine yapo katika hatua ya umaliziaji. Ifikapo tarehe 22/02/2021 tunataka madarasa hayo pamoja na samani zake yawe yamekabidhiwa”. Alisema

katika tukio hilo, Katibu Tawala  ametoa taarifa ya kufungiliwa kwa bwawa la Mtera linalomwaga maji yake mto rufiji kuwa limekaribia kujaa na kuwa muda wowote litafunguliwa. Kufuatia taarifa hiyo, amewataka madiwani na viongozi mbalimbali hususani wanaokaa kwenye maeneo ya maafuriko kuwatangazia wananchi wa maeneo hayo ili waanze kuchukua tahadhari mapema. “Tumepokea taarifa kuwa bwawa la Mtera linakaribia kujaa na wakati wowote litafunguliwa. Tuwataarifu wananchi wetu walipo maeneo ya maafuriko ili waanze kuchukua tahadhari mapema” alisema.

Pia ametoa taarifa ya kusimamishwa kwa uvunaji wa mazao ya misitu aina ya Mkuruti toka kwa wakala wa misitu TFS.

Kwa upande wake Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mbunge), amewataka Viongozi kuwaondoa wasiwasi Wananchi juu ya changamoto za barabara zilizochini ya TARURA na kueleza kuwa tayari Wabunge wameomba ongezeko la bajeti ya TARURA kufika asilimia 40 na kuwa tayari Serikali imelichukua na italifanyia kazi. “ Tuwaambie wananchi wetu wawe na subira wakati Serikali inaendelea kuangalia njia bora ya kutatua changamoto hizi.” Alisema.

Pia amewataka Watendaji kuchapa kazi kwa moyo na kuwa changamoto za kazi zinaendelea kufanyiwa kazi. “watendaji wetu niwaombe muendelee kuchapa kazi , tunatambua changamoto zenu nasi tunaendelea kuona namna tunaweza kuboresha maslahi yenu. Tumeshaanza kuiomba Serikali bungeni ili iweze kuwapandishia mishahara Watumishi wetu.” Alisema

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Juma Ligomba amesisitiza kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Korona ,  ukamilishaji wa vyumba vya madarasa pamoja na samani zake na kutoa tarehe ya kukabidhi kwa upande wa halmashauri kuwa ni tarehe 20 kabla ya tarehe ya Mkuu wa Wilaya. “ kwa upande wa Halmashauri tuhakikishe tunakamilisha ifikapo tarehe 20 illi Mkuu wa Wilaya anapokuja kukagua tarehe 22 akute tumejikamilisha.” Alisema

Pia amewataka viongozi na watendaji kukusanya mapato na kuchukulia suala hilo kama jicho na mchanga. “ ukusanyaji wa mapato katika Wilaya yetu uwe kama jicho na mchanga. Wote twendeni tukasimamie mapato. Mashine za kukusanya fedha zifuatliwe kwa ukaribu.” Alisema

Ligomba amewataka watendaji wa kata kuhakikisha wanashirikiana na wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji kuhakikisha wanafunzi wote watakao takiwa kwenda shuleni kuanzia tarehe 28/02/2021 wanakwenda na taarifa zao zinatolewa. “ Watendaji wa kata mkasimamie watoto wote waende shule. Mkashirikiane pamoja na Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji kuhakikisha suala hilo linatekelezwa na taarifa tuzipate.” Alisema.

Awali baraza lilipata fursa ya kusikiliza bajeti ya idara ya Maji Rufiji (RUWASA) iliyosomwa na Meneja wa idara hiyo  pamoja na taarifa za utekelezaji na mipango toka kwa Meneja wa TARURA wilayani Rufiji, huku wakipata nafasi ya kuuliza maswali, kutoa ushauri na kupata majibu toka kwa Viongozi hao.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • CHATANDA, MCHENGERWA WASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA MITANO YA BIL 13.3 YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA RUFIJI

    May 07, 2025
  • CHATANDA ARIDHISHWA NA KUPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

    May 08, 2025
  • KATIKA KIPINDI CHANGU CHA MIAKA 10, TUMEJENGA SHULE MPYA 20 ZA SEKONDARI' - MCHENGERWA. 1

    May 08, 2025
  • WAKUU WA DIVISHENI NA VITENGO RUFIJI WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS.

    April 28, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa