• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

RC KUNENGE: SERIKALI INATHAMINI MICHANGO YA WAFANYAKAZI KATIKA KULETA MAENDELEO

Posted on: May 1st, 2024


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amesema Serikali inathamini michango ya Wafanyakazi katika kuliletea Taifa maendeleo.

"Serikali inathamini michango ya  Wafanyakazi katika kuletea Taifa maendeleo" alisema.

Kunenge aliyasema hayo jana Mei 1, 2024  wakati akihutubia katika maadhimisho  ya Sikukuu ya Wafanyakazi  Mei Mosi  yaliyofanyika Kimkoa Wilayani Kibiti.

Ameeleza kuwa wafanyakazi wamekuwa wakifanya kazi za ziada zenye tija  zaidi ya zile walizopangiwa kufanya.  "Kazi nyingi za ziada wanafanya kwa uzalendo wao na ndizo zenye tija" amesema Kunenge.

Ameeleza kuwa Rais Dkt Samia anawapenda na kuwathamini sana Wafanyakazi wa mkoa wa Pwani, "Mhe Rais anangalia namna gani anaongeza uwezo wa serikali kuboresha mazingira ya kazi nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya shule ambazo watoto wanasoma, sekta ya afya na tayari ameahidi kuboresha makazi ya Wafanyakazi katika sekta ya elimu na afya" amesema Kunenge.

"Walimu mpate nyumba, Watu wa afya mpate nyumba na sehemu zingine tumeshaanza lakini wanasema unashona koti kulingana na ukubwa wa kitambaa ulichonacho huwezi kufanya mambo kama uwezo bado ni mdogo." Alisema Kunenge.

Alisema serikali inafahamu kazi kubwa inayofanywa na Wafanyakazi wa sekta, idara na Taasisi mbalimbali katika kuhudumia Wananchi na kumsaidia kazi Rais mkoani humo.

Hatahivyo Kunenge aliwataka Wafanyakazi mkoa wa Pwani kufanya kazi kwa bidii ilikuongeza tija katika utendaji kazi wao kwa Wananchi ili kuboresha maisha ya Wananchi mkoani Pwani.

Aidha aliwataka kuzungumzia kazi nzuri anazofanya Rais Dkt Samia katika kuhudumia Wananchi nchini "mnapopata nafasi semeni mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye anawapenda na kuwajali Wafanyakazi nchini kwani anawahakikishia usalama, haki za Wafanyakazi kazini

Akizungumzia changamoto mbalimbali walizoziwasilisha kupitia risala ya Wafanyakazi Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani alisema Kuna masuala mengi tayari yanafanyiwa kazi ikiwemo  suala la kikokotoo cha wastaafu.

Awali Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania TUCTA mkoa wa Pwani Kinyogoli Ramadhani ameomba serikali kuangalia namna ya kusaidia usafiri wa uhakika kwa Walimu wanaofundisha katika Shule za maeneo ya Kata za Delta ambako kutoka sehemu Moja kwenda nyingine hutumia


Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA AMWAGA BIL. 50 BARABARA YA IKWIRIRI -MKONGO

    June 23, 2025
  • DC KOMBA AAGIZA ELIMU YA MABADILIKO YA TABIANCHI ITOLEWE KWA KATA ZOTE RUFIJI.

    June 26, 2025
  • WATUMISHI WA UMMA RUFIJI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI, WASISITIZWA KUFANYAKAZI KWA BIDII, WAONYWA KUTOA HUDUMA KWA UPENDELEO MAOFISNI

    June 25, 2025
  • BEREGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA MKONGO, KIPUGIRA, NGORONGO

    June 11, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa