• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

MRADI WA KILIMO CHA PAMBA WAZINDULIWA RUFIJI.

Posted on: January 13th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amewataka Wanachi wa Rufiji kuchangamkia fursa ya kulima kilimo cha Pamba kwa kuwa zao hilo litakwenda kusaidia kukuza kipato chao.

Kunenge ameyazungumza hayo jana Januari 13, 2024 kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa kilimo cha Pamba ambao upo chini ya uwekezaji wa Kampuni ya ‘RUFIJI COTTON LTD’ iliyofanyika katika Kijiji cha Chumbi A, Kata ya Chumbi Wilayani Rufiji.

“Mwekezaji amesema kiwanda atakachojenga uzalishaji wake hautoshelezi na nyie ndio Soko,  na wengi ambao tumepata matatizo huko nyuma ni kwasababu ya masoko. Mimi naamini kupitia kilimo cha Pamba maisha yenu yanakwenda kutabadilika, kwasabau unalima na unauza hapohapo”.

Pia RC Kunenge amesema  juhudi zinazofanywa na Serikali za kuweka sera na mazingira mazuri ya uwekezaji ni kuona Mwananchi wa chini anaguswa na miradi kama hiyo  na ananyanyuka kiuchumi.

Akizungumzia hali ya uwekezaji, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya uwekezaji wa Pamba Rufiji ‘Rufiji Cotton Ltd’ Hassan Kaunje, amesema wameamua kuwekeza Rufiji kwasababu ya mazingira mazuri ya Wilaya ya Rufiji na mapokezi mazuri ya Wananchi wa Chumbi pamoja na Serikali.

“tumekuja kulima na Wanarufiji sio kununua pamba, tunaanza kulima nao katika hatua ya kwanza, ndio maana Mhe. Mkuu wa Mkoa mbele yako unaona vifaa vya kilimo matrekta, madawa na pikipiki. Kwahiyo huduma za kilimo za matrekta na kila kitu zitalipiwa na Kampuni ya Rufiji Cotton Ltd.

Tumeajiri Maafisa Ugani 24 watakaoenda katika vijiji vyote 24 vitakavyolima Pamba, tumewapa na Vifaa (pikipiki). Itakapofika mwezi wa sita mwaka huu tutakuwa na Kiwanada cha kuchambua Pamba ambacho kitajengwa katika Kijiji cha Chumbi na baada ya kumaliza tutaichukua Pamba na kuipeleka India kwenye Viwanda vyetu” amesema Kaunje.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowele amesema kwa Kushirikiana na Bodi ya Pamba Wamepita katika Vijiji vyote 24 kuhamasisha kilimo cha Pamba hali anayoamini italeta matokea chanya kutokana na muitikio mzuri wa Wananchi huku akiwahakikishia Wawekezaji kuwa Rufiji ni sehemu salama na ina maeneo mazuri ya uwekezaji.

“Mimi ni kuhakikishie Wilaya hii ipo salama sana, hata Wawekezaji wanaokuja tumewakikishia usalama wao na Watawekeza katika mazingira ambayo ni salama, niombe pale Mtakapopata Wawekezaji wengine naomba Mtuletee Rufiji, sisi tumeamua tuunge mkono juhudi za Rais za kusapoti uwekezaji” amesema Gowele.

Akitoa salamu za Wananchi Diwani wa Kata ya Chumbi Ally Nguyu amesema Wananchi wa Chumbi kwa umoja wao  kwenye vikao vya ndani na mikutano mikuu ya Vijiji walikubali kutoa hekari 6000 kwa ajili uwekezaji.

“Wanachumbi hawa kwa umoja wao Chumbi A, B na C kwa umoja wao kwenye Vikao vya ndani na Mikutano mikuu wa Vijiji waliridhia kutoa hekari 6000 kwa muwekezaji huyu. Niwaombe Wanachi wenzangu wa Chumbi na Rufiji yote tuungane kwa pamoja kama neema ndio hii” amesema.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Marco Mtunga amewapongeza Wananchi wa Chumbi kwa kumkubali muwekezaji huyo huku akibainisha kuwa ziara ya Rais India ndio imekuwa chachu kwa muwekezaji huyo.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • BEREGE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATA YA MKONGO, KIPUGIRA, NGORONGO

    June 11, 2025
  • BEREGE AKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA MOHORO.

    May 29, 2025
  • WAKUSANYA KODI RUFIJI WAPEWA MAFUNZO UKUSANYAJI WA KODI YA MAJENGO, PANGO LA ARDHI NA USHURU WA MABANGO.

    May 26, 2025
  • BEREGE AWATAKA WAFANYABIASHARA RUFIJI KUANZA KUJIANDAA NA KUZITUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI

    May 21, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa