• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Rufiji District Council
Rufiji District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
      • ladi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara na Vitengo
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Work and Fire Rescue
      • Ardhi na Maliasili
      • Mazingira
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji na Umwagiliaji
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma ya maji safi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Fedhda, Utawala na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Social Services
      • Maadili
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa vyombo vya habari

MKURUGENZI RUFIJI KUKABIDHIWA SHULE MPYA

Posted on: November 13th, 2020


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Ndg. Rashid Salum Salum amekabidhiwa Shule Mpya na Mkurugenzi wa Taasisi ya African Relief iliyojengwa kwa msaada wa watu wa Kuwait chini ya usimamizi wa taasisi hiyo. Tukio hilo limeshuhudiwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania ambaye aliambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luteni Kanali Patrick Sawala pamoja na Wananchi wa Kitongoji cha Kanga, Kijiji cha Chumbi C, Wilayani humo. Shule hiyo imejengwa kwa lengo la kusaidia Wanafunzi wa  elimu ya Msingi ambao walikuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kufika Shuleni.

Akizungumza na Wanachi pamoja na Wageni Mbalimbali waliohudhuria tukio hilo, Mkuu wa Wilaya amemshukuru Balozi wa Kuwait nchini Tanzania kwa kuhudhuria  tukio hilo na kuacha majukumu mengine ya Kitaifa. Pia amemshukuru kwa msaada unaotoka kwa moja ya Wananchi wa Kuwait na kuchagua Tanzania hususani Rufiji kuwa sehemu ya kutoa msaada huo.” Hii inaonesha ni jinsi gani Serikali ya Tanzania chini ya Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli inamahusiano mazuri na mataifa mengine” Alisema.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwashukuru Wananchi na Kuwapongeza kwa kuendesha uchaguzi uliokuwa wa amani na utulivu mkubwa na kuwataka Wanachi hao kuendeleza amani hiyo ili kuweza kujikita katika mambo ya kimaendeleo. “ kama alivyosema Mhe. Rais kuwa uchagiz umekwisha na sasa tuchape kazi” Alisema.

Sambamba na hayo amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Rufiji kusimamia Usajili mapema ili kufikia januari wanafunzi wa Kitongoji hicho waanze kusoma katika Shule hiyo. Pia amewataka Wazazi na Walezi wenye watoto waliotimiza umri wa kuanza Shule kuhakikisha Wanawaandikisha watoto wao mapema iwezekenavyo.

Kwa upande wake Balozi wa Kuwait nchini Tanzania ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania hasa Wilaya ya Rufiji na kuongeza kuwa ataendelea kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ili kuendelea kutatua changamoto zinazoikabili Wilaya hiyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya African Relief amesema bado taasisi yake itaendelea kuichagua Rufiji kuwa sehemu ya kushirikiana na Wananchi kutatua changamoto kama ilivyokuwa hapo awali.

Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Rufiji Ndg. Rashi Salum Salum ameishukuru Taasisi ya African Relief kwa kuendeleza ushirikiano na kutoa misaada kwa Wananchi wa Rufiji hususani wale waliokatika mazingira magumu zaidi na kuahidi kuwa kwa Shule hiyo aliyokabidhiwa atasimamia usajili kwa haraka kama alivyoagizwa na Mkuu wa Wilaya.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAHILI RUFIJI December 28, 2023
  • TANGAZO LA MNADA May 21, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 17, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI September 17, 2024
  • Ona zote

Habari Mpya

  • BEREGE AKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KATA YA MOHORO.

    May 29, 2025
  • WAKUSANYA KODI RUFIJI WAPEWA MAFUNZO UKUSANYAJI WA KODI YA MAJENGO, PANGO LA ARDHI NA USHURU WA MABANGO.

    May 26, 2025
  • BEREGE AWATAKA WAFANYABIASHARA RUFIJI KUANZA KUJIANDAA NA KUZITUMIA FURSA ZA UWEKEZAJI

    May 21, 2025
  • UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA CHIKICHI KUTOA AJIRA 5,000.

    May 16, 2025
  • Ona zote

Video

Viwanja vinauzwa Mparange Ikwiriri Wialayani Rufiji
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Bima ya Afya ya Taifa
  • Fomu ya Uhamisho wa Mwanafunzi wa Sekondari

Tovuti Linganifu

  • Tovuti ya Serikali - Tanzania
  • OR-Tamisemi
  • Utumishi wa umma
  • Tovuti ya Mkoa wa Pwani
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    MKURUGENZI MTENDAJI(W),

    Anwani ya Posta: S.L.P 28 UTETE/RUFIJI

    Simu ya Mezani: 0232010304

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: ded@rufijidc.go.tz

Mawasiliano mbadala

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©Ded-RufijiDC 2017 Haki zote Zimehifadhiwa